Aliyekuwa Kocha wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera, amewataka mabosi kumlipa fedha zake ambazo anadai ndani ya wiki moja.
Zahera ambaye ni raia wa Congo, amesema ametoa wiki moja pekee na wasipofanya hivyo ataenda FIFA kushtaki.
Zahera ambaye alifutwa kazi hivi karibuni kufuatia kufuatia kuwa na mwenendo mbaya wa matokeo, ameeleza kutopewa fedha ambazo alikuwa anaikopesha Yanga kutokana na kupitia kipindi kigumu.
Fedha zinajumuisha zile za mihshara ya wachezaji, kulipia nauli ya safari kadhaa za ndege, hela za chakula kwa wachezaji na zinginezo.
Kocha huyo mpaka sasa yupo hapa nchini akiendelea kusubiria fedha hizo ambazo bado anazidao Yanga.








Mwinyi Zahera usiondoke bila kulipwa na hao vyura.
ReplyDeleteWasamehe tu papaa maana hali yao siyo nzuri kiuchumi!yaani mpaka huruma jamani
ReplyDeleteHawana shukurani. Wadai haki yako. Kwani licha ya kuwasimamia kwa hali na mali wameshindwa kuonyesha uungwana.
ReplyDeleteWamlipe asiondoke hyo ni haki yake
ReplyDelete