January 22, 2020


Baada ya ushindi wa juzi wa mabao 4-1 dhidi ya Alliance FC katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara uliochezwa kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini hapa, Kocha Mkuu wa Simba, Sven Vanderbroeck amesema kwa sasa lengo lake kubwa ni kuchukua ubingwa.

Alisema ana imani kubwa na timu yake itafanya hivyo kutokana na ubora wa kikosi walichonacho.
Akielezea kuhusu mchezo wao na Alliance FC, Sven alisema timu yake ilianza vyema kwa kucheza mchezo safi licha ya kuruhusu bao katika dakika ya 28.

Kocha huyo wa zamani wa timu ya taifa ya Zambia alisema anawapongeza wachezaji wake kwa kuweza kusawazisha kabla ya mapumziko.

Akielezea kuhusu ligi hiyo, Sven alisema ni ngumu na kila timu inajitaidi kucheza soka safi la kuvutia ili iweze kupata matokeo mazuri.

Alisema kwa sasa atahakikisha wanatwaa ubingwa wa Ligi Kuu ili Simba iweze kucheza tena Ligi yua Mabingwa wa Afrika.

Kwa upande wake, Kocha Mkuu wa Alliance FC, Fredy Minziro alisema timu yake ilianza kwa kucheza vyema, lakini ilifanya makosa ndio wapinzani wao wakaweza kusawazisha na kuwafunga.
Alisema kwa sasa watarekebisha makosa yaliojitokeza ili timu yao iweze kushinda michezo ijayo. Simba SC mpaka sasa bado inaongoza msimamo wa ligi hiyo ikiwa na pointi 41.

Timu hiyo imeshinda mechi 14, sare mbili na imepoteza mechi moja tu dhidi ya Mwadui FC

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic