January 15, 2020

YUSUPH Mhilu mshambuliaji wa Kagera Sugar leo amekiongoza kikosi chake kuingamiza Yanga kwa mabao 3-0 kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa leo, Januari,15, Uwanja wa Uhuru.

Mhilu alifungua akaunti ya mabao dakika ya 13 kwa kuachia shuti kali lililomshinda mlinda mlango Farouk Shikalo.

Yanga ikiwa chini ya nahodha wao Haruna Niyonzima kwenye mchezo wa leo ilimshuhudia kiungo wao Mohamed Issa 'Mo Banka' akiwapunguzia kasi dakika ya 44 baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kutokana na kuonyeshwa kadi mbili za njano kwa kucheza faulo kwa wachezaji wa Kagera Sugar.

Kipindi cha kwanza Yanga walikwenda mapumziko wakiwa nyuma kwa bao 1-0 walijipanga kurejea kupindua meza kipindi cha pili mambo yakazidi kuwa magumu kwani Kagera Sugar iliyo chini ya Mecky Maxime ilimzidi ujanja Luc Eymael ambaye ni mara yake ya kwanza kukaa kwenye benchi la ufundi akipokea kijiti cha Mwinyi Zahera.

Bao la pili kwa Kagera Sugar lilifungwa dakika ya 66 kupitia kwa Ally Ramadhan aliyemalizia pasi ya Abdallah Siseme na msumari wa mwisho ulipachikwa kwa kichwa dakika ya 89 na kuifanya Yanga kushindwa kutumia dakika nne za nyongeza kupata bao la kufutia machozi.

Kagera Sugar imecheza jumla ya mechi 17 inafikisha jumla ya pointi 27 inapanda mpaka nafasi ya nn, Yanga inakuwa nafasi ya nane ikiwa imecheza jumla ya mechi 13 na ina pointi 25 kibindoni.

14 COMMENTS:

  1. Hakuna timu hapo vyura wa jangwani

    ReplyDelete
  2. Gunia la msumari hawa bebeki hata siku moja

    ReplyDelete
  3. kocha wa salehe Jembe alimsifia sana zlipoanza..eti ana CV ya kutosha..Hakuna timu anakaa mwaka. Yanga wamempa mwaka na nusu!Timu anzofundisha zinashika nafasi 14 au 16..Yanga leo imeshuka hadi 13..Kombe la premium ligi mara ya mwisho kachukua 2010 hadi 2011..

    ReplyDelete
  4. This comment has been removed by the author.

    ReplyDelete
  5. Ombi lako AL Hashimi la goli tatu limetekelezwa kama ulivotaka. Hongera ndugu

    ReplyDelete
  6. ndiomana hata mchezaji mpya jangwan tunabaki kuambiwa timu alizochezea wala sio kuwa yanga wamemsajili kutoka timu gani duuuu bongo bana

    ReplyDelete
  7. Hawoooooo kandambiliiiiiii vyuraaaaaaaa haoooooo

    ReplyDelete
  8. Simba Yanga zina mashabiki wa hovyo kwani kiuhalisia Yanga hii bado ni ya Mkwasa na Simba ya kombe la Mapinduzi bado ni ya Ausems kuwalaumu hawa makocha wapya ni kuwaonea.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hata kusajili zaidi ya wachezaji kumi ni presha ya mashabiki tu. Makocha hawasikilizwi mahitaji yao. Mfano timu unaiona inahitaji defensive midfielder lakini wataletwa attacking midfielders zaidi ya watano.

      Delete
  9. Ila Yanga wameekeza kunako propaganda zaidi kuliko uhalisia wa ubora wa timu yao. Kumaliza nguvu zote ili kutoa sare na simba hakuifanyi Yanga kuwa timu bora.

    ReplyDelete
  10. Kiukweli Yanga inahitaji kiungo mkabaji halisia hao, Banka, balama, tshishimbi, makame wote ni watu wa attacking sasa nashangaa yanga wameelekeza nguvu kwenye foward lakin hata huku defensive sasa hivi Yondani anachezea ozoefu, hao ni pamoja na nyoni, wawa hao wamebaki kuchezea ozoefu lakini bampa to bampa hawaezi kuendana na kasi ya vijana, na hii yote ni kuaminishwa haya na viungo ni wale wale usajili umefungwa mechi ya kukamia imebaki moja na azami simba mlikamia mkamaliza twende kazi. mahesabu yatajulikana May.

    ReplyDelete
  11. Kuna chura anaitwa Konaball mbona ha comment ?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic