KOCHA Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, amesema kuwa kuna tatizo linaloimaliza safu ya ulinzi taratibu na inahitaji kutafutiwa dawa mapema.
Yanga ikiwa imecheza jumla ya mechi 15, imefungwa mabao 15, sawa na idadi ya mabao iliyofunga kwa sasa.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Eymael alisema kuwa malengo yake ndani ya timu ni kuona inashinda na kupata matokeo Ila bado kuna tatizo kwenye safu ya ulinzi.
“Mechi nne nimeshudia tulipoteza kwa kufungwa mabao 3-0 na Kagera Sugar, tukafungwa na Azam FC bao 1-0 pia hata tuliposhinda mabao matatu mbele ya Singida United tulifungwa bao moja kuna namna ya kulimaliza hili tatizo nitawapa mbinu mpya wachezaji,” alisema Luc.
0 COMMENTS:
Post a Comment