JURGEN Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amemzidi mbinu mpinzani wake Ole Gunnar Solksjaer wa Manchester United kwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu England.
Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Anfield, Liverpool wakiwa nyumbani ulikuwa ni wa ushindani na wengi walitarajia kuona mabao mengi mwisho wa siku ni mabao mawili yalipatikana.
Liverpool inazidi kuongeza nguvu za kuufukuzia ubingwa kutokana na kushindikana kupoteza mechi ilizocheza mpaka sasa kwenye ligi,
Bao la kwanza kwa Liverpool lilifungwa na beki kisiki, Virgil Dijk dakika ya 14 kipindi cha kwanza kwa kichwa na bao la pili lilifungwa na Mohamed Salah dakika ya 90+3.
Ushindi huo unaifanya Liverpool kujikita kileleni ikiwa na jumla ya pointi 64 ikiwa imecheza jumla ya mechi 22 huku mabingwa watetezi Manchester City wakiwa nafasi ya pili na pointi 47, United ipo nafasi ya tano na pointi 34 imecheza mechi 23.
Mchezo wa kwanza ulipokuwatanisha wababe hawa ngoma ilitoka sare ya kufungana bao 1-1.
0 COMMENTS:
Post a Comment