GERALD Mdamu, mshambuliaji wa Mwadui FC amekuwa ni mwiba kwa makipa wote wa kikosi cha kwanza cha Simba kwa kuwatungua wote mabao kila wanapokutana uwanjani.
Mdamu mwenye jumla ya mabao manne ndani ya Ligi Kuu Bara, alianza kumtungua Aish Manula ambaye ni mlinda mlango namba moja ndani ya Simba kwenye mechi ya ligi iliyochezwa uwanja wa Kambarage, Shinyanga kwa kichwa wakati Simba ikipoteza kwa kufungwa bao 1-0.
Manula akiwa amecheza jumla ya mechi 13 amefungwa jumla ya mabao matano huku moja akitunguliwa na Mdamu kwa kichwa ndani ya 18. Balaa lake alilihamishia kwa Beno Kakolanya kwenye mchezo wa Kombe la Shirikishouliochezwa Uwanja wa Taifa wakati Simba ikishinda mabao 2-1.
Bao pekee la Mwadui FC lilipachikiwa kimiani na Mdamu na kufanya kuwa mwiba kwa walinda mlango wote wa Simba ambao ni tegemeo kwenye kikosi cha kwanza.
Mdamu ameliambia SpotiXtra kuwa kikubwa anachokifanya akiwa uwanjani ni kupambani timu yake kupata matokeo.
0 COMMENTS:
Post a Comment