January 5, 2020


RASMI sasa kiungo wa Mamelodi Sundowns, Luis Jose Miquissone aliyekuwa anakipiga kwa mkopo UD Songo ya Msumbiji ni mchezaji halali wa Simba baada ya kufanikiwa kumsainisha mkataba wa miaka miwili.

Usajili wa kiungo wa kwanza kwa Simba tangu lifunguliwe dirisha hili dogo lililofunguliwa tangu Desemba 16, mwaka jana ambalo litafungwa Januari 15, mwaka huu.

Simba imefanikisha usajili huo baada ya kuwazidi ujanja watani wao wa jadi, Yanga ambao ilielezwa ilikuwepo kwenye mazungumzo ya kukamilisha usajili wake kabla ya kumsajili kiungo Mnyarwanda Haruna Niyonzima aliyekuwa anakipiga AS Kigali ya Rwanda.


Kwa mujibu wa mtandao wa klabu hiyo ya Simba, kiungo huyo wamefikia makubaliano mazuri na timu hiyo kabla ya kusaini mkataba wa kuichezea timu hiyo ikielezwa atakipiga Msimbazi kwa muda wa miaka miwili.

Kiungo huyo jana mchana alikabidhiwa jezi na kocha mpya wa timu hiyo, Mbelgiji Sven Vandenbroeck ambaye alimkaribisha mara baada ya kutua nchini usiku wa kuamkia jana akitokea Afrika Kusini.

Luis mara baada ya kumalizana na viongozi wa Simba, jana alikabidhiwa ishara ya kuwa tayari ni mchezaji halali wa timu hiyo ambaye huenda akawa sehemu ya kikosi cha timu hiyo kitakachoivaa Yanga katika pambano la Kariakoo Derby.

Kutua kwa kiungo huyo kutaimarisha safu ya viungo katika timu hiyo ambayo tayari ina Francis Kahata, Clatous Chama, Mzamiru Yassin, Gerson Fraga, Hassan Dilunga, Said Ndemla, Sharraf Shiboub, Ibrahim Ajibu na Jonas Mkude.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic