January 28, 2020

THOMAS Ulimwengu, mshambuliaji wa timu ya Taifa ya Tanzania aliyekuwa anakipiga kwenye klabu ya JS Saura ya Algeria yupo kwenye hatua za mwisho kutambulishwa ndani ya TP Mazembe.

Ulimwengu alicheza timu hiyo ya TP Mazembe ambayo ni miongoni mwa klabu zenye ushindani Afrika ndani ya Ligi ya Mabigwa Afrika amejiunga na Klabu yake ya zamani ya TP Mazembe aliyesepa klabuni hapo 2016.

Ulimwengu alicheza na nyota bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani 2016, Mbwana Samatta anayekipiga kwa sasa ndani ya Aston Villa inayoshiriki Ligi Kuu ya England.


Taarifa zinaeleza kuwa nyota huyo aliyekuwa anakipiga JS Saoura amesaini kandarasi ya miaka miwili na anaweza kutambulishwa kesho Januari 29 ama 30 mambo yakiwa sawa.

Kwa sasa Ulimwengu yupo Bongo akikamilisha taratibu za mwisho kabla ya kujiunga na klabu yake hiyo ya zamani.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic