KIUNGO Mshambuliaji wa Simba, Hassan Dilunga amesema kuwa
wachezaji wamekubaliana kupambana mwanzo mwisho mpaka kulitwaa taji la Kombe la
Shirikisho kutokana na uwezo walionano.
Simba imetinga hatua ya 16 bora kwa ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Mwadui uliochezwa Uwanja wa Taifa,
juzi kiungo huyo alikuwa msumbufu kwa mabeki wa Mwadui na alisababisha faulo
tano kati ya 12 walizochezewa na Mwadui.
Dilunga amesema kuwa
ushindani ni mkubwa jambo linalowafanya nao wapambane kupata matokeo kwenye
mechi zao zinazofuata na hakitaeleweka mpaka watwae taji.
“ Ushindani ni mkubwa kila timu inapambana kupata matokeo kwa
hatua ambayo tumefikia bado tuna kazi ya kufanya, ili kieleweke tutafurahi tukitwaa
taji kwani kila mchezaji ni furaha yake kuona tunafikia malengo hayo,” amesema
Dilunga.
Hatua ya 16 bora Simba itamenyana na Stand United inayoshiriki Ligi Daraja la Kwanza, tarehe ya mchezo huo bado haijapangwa.
0 COMMENTS:
Post a Comment