January 31, 2020


Baada ya kuonyesha vitu adimu vilivyomkosha kila Mwanayanga na kuwaumiza wapinzani, straika wa Yanga, Bernard Morrison, ameingia chimbo kutengeneza dawa ya mabeki jeuri.

Morrison aliyetua Yanga katika usajili wa dirisha dogo, amekuwa gumzo kutokana na mbwembwe zake za kuchezea mpira maarufu kama Shobobo.

Katika mechi mbili pekee alizocheza dhidi ya Singida United na Tanzania Prisons, tayari amedhirisha kuwa na kiwango bora, kwani pamoja na kutoa burudani, ameisadia timu yake kupata ushindi.

Sasa kwa taarifa yao wale wanaumizwa na miondoko yake uwanjani, wajiandae kuona vitu vingine vipya na safari hii mabeki wajipange.

Baada ya michezo miwili aliyocheza, Morrison amebaini kuna mabeki wabishi na watamkamia katika mechi zijazo, hivyo ameamua kujifungia ndani kupitia video za michezo yote ya timu za Ligi Kuu Tanzania Bara.

Morrison ameeleza kuwa kwa kipindi walichopewa mapumziko, anakuwa bize kuangalia video za mechi mbalimbali za Ligi Kuu Bara ili kubaini aina ya uchezaji wa mabeki atakaokabiliana nao.

“Nimeona ni vizuri kupitia video za timu nitakazocheza nazo, nipate vitu vitavyonisaidia uwanjani, najua safari hii mabeki watakuwa wamejipanga kukabiliana na mimi,’ alisema winga huyo raia wa Ghana.

Katika mechi mbili alizocheza, nyota huyo wa Yanga amefunga bao moja na kutengeza nafasi za mabao mawili ‘assists’. 

9 COMMENTS:

  1. Nani hao unaowkusudia kuwa wataoona uchungu hebu wataje. Maneno kama hayo ndio yanayokufikisheni msikokupenda

    ReplyDelete
  2. Wewe kwa mwenye akili timamu nani anajali ujinga anaoufanya huyo kijana. Kwa nafasi ya Yanga kwenye ligi anachokiremba kitu gani?

    ReplyDelete
  3. Huyo mchezaji mwenyewe kakalia kishoga..samahani kakalia kishobo vile vile. Inawezekana kuna kidume kimemficha.

    ReplyDelete
  4. Mechi mbili asisst mbili na goli moja haitoshi kuonesha kwamba huyo mchezaji ana kitu flani? Kwa wanaobeza na kukejeli inaonesha kweli roho zinaumia.

    ReplyDelete
  5. Enter your comment...kiukweli jamaa yupo vizuri mi nashangaa wanaombeza cha msingi aongeze juhudi tu na asilewe sifa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hana uwezo kumpita mapinduzi balama, na nashangaa kuwa anapambwa mno

      Delete
  6. Unajua wapenzi wa Simba wengi ni mabwabwa,hivyo sishangai wakimponda

    ReplyDelete
  7. Kizuri hakikosi kupigwa mawe jamaaa mzurii ushabiki pembeni

    ReplyDelete
  8. Mzuri kama mdada au mzuri kivipi?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic