SVEN Vandenboeck, Kocha Mkuu wa Simba raia wa Ubelgiji ana mechi
tatu za ligi sawa na dakika 270 za moto ndani ya Simba kuweka rekodi yake mpya
kutokana na ugumu wa mechi zake zilizobaki.
Simba ikiwa nafasi ya kwanza kwenye ligi na pointi zake 41
imecheza mechi 16 imebakiza mechi tatu kukamilisha mzunguko wa kwanza ambazo
zote ni za moto kwa Sven kuweka rekodi yake mpya ndani ya mechi zake tisa za
awali.
Endapo atashinda mechi zake zote tatu zilizobaki ama kulazimisha
sare ndani ya mechi hizo atapindua meza kibabe na kuipoteza rekodi ya
mtangulizi wake Patrick Aussems ambaye kwenye mechi zake tisa za mwanzo
alipoteza mechi yake ya nne mbele ya Mbao FC kwa kufungwa bao 1-0.
Mechi zake tatu zilizobaki ni dhidi ya Coastal Union ya Tanga
iliyo chini ya Juma Mgunda, Namungo ya Lindi iliyo chini ya Thiery
Hitimana na Polisi Tanzania ya Moshi
iliyo chini ya Malale Hamsini.
0 COMMENTS:
Post a Comment