Kocha na mchezaji wa zamani wa Simba, Jamhuri Kihwelo 'Julio' ameibuka na kusema kuwa Kocha mpya waliyemsajili Yanga, Luc Eymael, anaweza akaipeleka pabaya timu hiyo badala ya kuipa mafanikio.
Julio ameeleza kuwa Yanga ni kama wamekurupuka kufanya usajili wa Eymael kutokana na timu ilikuwa imeshaanza kurejea kwenye morali kama zamani.
Amefunguka kwa kushangazwa na namna Yanga ambavyo wamefanya haraka kutafuta kocha mwingine badala ya kumuachia Boniface Mkwasa majukumu ya kuendelea na kazi walau mpaka mwisho wa msimu huu.
Julio amesema Yanga ni kama wameuziwa mbuzi kwenye gunia, anaamini Aymael si sahihi ndani ya timu na hilo ameeleza limechagizwa na kupoteza mechi zake mbili za mwanzo, sambamba na kauli ya ubaguzi aliyoisema baada ya kupoteza dhidi ya Azam FC.
"Hawa Yanga naweza kusema ni kama wameuziwa mbuzi kwenye gunia, hauwezi kumleta kocha mwingine wakati timu imeshaanza kuonesha mwanga mzuri.
"Katika kipindi kama hiki walipaswa kumuachia Mkwasa timu aende nayo walau mpaka mwisho mwa msimu huu".
Julio uko sahihi kabisa hawa Watani zetu walikurupuka tu
ReplyDeleteMbali na Kocha, Yanga kosa la pili kubwa ni kwa wakati mmoja kukibadilisha kikosi kwa asilimia kubwa ili wahakikishe ubingwa ni wao mapema na kujikuta wachezaji hawajuwani pamoja na Kocha wao mpya vilevile kila mmoja kivyake ikajikuta timu huyu akenda kusini huyu anaekekea kaskazini na huku mabadiliko Katika uongozi
ReplyDeleteUkweli ndio huo ni makosa makubwa sana kubadilisha timu nzima na ndio kitu kinachowagharimu sasa.
DeleteKwa kuwa wachezaji waliosajiliwa ni wazuri, na Kocha ni wa viwango hakuna tatizo, kinachosubiriwa ni wachezaji kuzoeana na kutengeneza muunganiko mzuri. Ni suala la muda tu, matokeo haya mabaya ni kipindi kifupi Cha mpito. Usajili uliofanywa unaashiria kwamba Yanga itatisha Sana.
ReplyDeleteKaka unaakili Sana unajua hawa mikia wanatuwaza Sana maana kila kitu lazima waseme ukweli nikwamba tunamshukuru mkwasa lakini sio kocha wakutuletea jipya wao wanyamaze wasituingilie pumbavu Julio fala tu anashauri nn kwann asiwashauri simba kutomsajili kichuya Kama anaakili??
DeleteHayo ni maoni ya Pastory Kyombya
ReplyDeleteWewew JULIO Una shauri il iweje mtu mwenyewe huna timu mpaka leo halaf unategemea ushauri wako utakuwa na tija,unataka nawewe kupata umaarufu kupitia yanga....acha ngenga wafuatilie mikia fc
ReplyDeleteToka lini Paka aka mshauri panya, Yanga ipo kwenye kipindi Cha mpito, itaimarika na watu watasahau, Ni suala la muda tu, hata hao wanaojiona wako vizuri, mfadhili wa anatafuta sababu ya kujitoa, wasubirie kivumbi kwenye Twitter..
ReplyDeleteYanga iko vizuri sana Ila inawezekana kunawatu wachache tu wanao hujumu timu ili kocha mpya aonekane afai ,Ila inabidi wakazane ili washike angalau nafasi ya pili maana mnyama yupo full nondo na ubingwa Ni wake Kama kawa
ReplyDeleteKwani huyo julio yy nae si ni kocha !anautoa wapi ujasili wa kuongea wakati hata timu ya kufundisha hana!aende akawashauri mikia wenzie au akacheze kiduku kama alivozoea
ReplyDeleteJulio yake yanamshinda yet atayaweza .
ReplyDelete