January 20, 2020


JUMA Abdul, nahodha msaidizi wa Yanga kuwa watapambana kwenye mechi zao zilizobaki kutokana na kutokuwa na matokeo mazuri kwenye mechi zao mbili za hivi karibuni.

Yanga ilipoteza mbele ya Kagera Sugar kwa kufungwa mabao 3-0 ikapoteza pia mbele ya Azam FC kwa kufungwa bao 1-0 mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Singida United utakaochezwa Jumatano, Januari, 22 Uwanja wa Namfua.

Abdul amesema:" Ahsanteni mashabiki wetu kwa kuja na tunawaomba tusikate tamaa tumepoteza mchezo wa pili mapambano bado yanaendelea tutafanyia kazi makosa yetu,".

Yanga ipo nafasi ya nane kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 25 baada ya kucheza mechi 14 itamenyana na Singida United iliyo nafasi ya 19 na pointi 10.

11 COMMENTS:

  1. Acha kujifariji inawezekana mkashinda kama mlivyoshinda mechi ya Simba,tumeshawazoea suluhu kwenu ndio ushindi.

    ReplyDelete
  2. Kufungwa Ni sehemu ya mchezo, tatizo Mashabiki wa mihemko ndio wanataka kushinda kila mechi, hakuna team ya namna hiyo duniani.

    ReplyDelete
  3. Nani amekwambia kwamba ligi imeisha?tatizo mwenendo wa timu acha kusema eti kufungwa ni sehemu ya mchezo,hakuna kiru kama hicho yanga kuna mauza uza mengi sana na kama hayatafanyiwa kazi basi tutabakia kua mabingwa wa kihistoria.chamsing tukubali udhaifu na tuufanyie kazi.

    ReplyDelete
  4. Droo ndio ushindi kwenu vyura nyinyi kandambili

    ReplyDelete
    Replies
    1. Wewe si mkweli wachache Yanga wao wenyewe watatue matatizo yao wenyewe kwa amani wakiishi kauli mbiu....daima mbele nyuma mwiko

      Delete
  5. Kwa singida ni draw au watani wanafungwa 1 - 0
    Subirini ijumaatano.

    ReplyDelete
  6. Sina hata hamu ya matokeo,hata tumfunge goli 100 hamna jipya

    ReplyDelete
  7. Ha ha ha ha ha watani bhana mna nipa raha sana ila ngoja tusubiri matokeo,mnashinda goli moja ila mkizubaa mnatoa suluhu.

    ReplyDelete
  8. ikifungwa bacca madrid man mancity ni kawaida ila ikifungwa yanga na simba haiwezekan mashabiki wa bongo jinga sna

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic