HARUNA Niyonzima
amesema matokeo ya sare nne mfululizo ndani ya ligi kuu,
yamewanyima vitu vingi, mbali ya kuwa katika nafasi finyu ya kuwa mabingwa pia wamepishana na milioni 40 kutoka kwa GSM, ambazo wangepata kama
wangeshinda michezo yote.
Niyonzima amesema wachezaji wote
wanaumia kwa kupata sare, kwani wao soka ndiyo kitu
kinachoendesha maisha na kuhudumia familia zao, kwa kuwa wamekuwa wakiingiza
shilingi miloni 10, kila wanaposhinda mechi, hivyo kukosa ushindi katika mechi
nne mfululizo kunafanya wapitie kipindi kigumu.
Ikumbukwe kuwa, kampuni ya GSM,
ilitoa ahadi ya kutoa shilingi milioni 10 kwenda kwa wachezaji wa Yanga, kwenye
kila mchezo ambao watakuwa wanashinda, jambo ambalo wamekuwa wakilikitimiza
kila wanaposhinda mchezo.
Akizungumzu na Championi Jumatano
Niyonzima alisema: “Kiukweli sisi kama wachezaji tunapitia kipindi kigumu sana
kwa sasa, kwa kuwa soka ndiyo kazi yetu inayoendesha familia zetu, ukumbuke
kuna milioni 10 za mdhamini ambazo huwa tunapata ikitokea tumeshinda mchezo,
michezo minne imepita hatujashinda, unaweza ukaona hapo tumekosa fedha kiasi
gani.
“Lakini tunaamini kuwa hiki
ni kipindi cha mpito tunapitia, kwa sababu timu yetu inacheza vizuri, ila
tumekuwa tukikosa matokeo tunayotaka, mashabiki wetu wasikate tamaa, tutakaa
sawa na tutakuwa tunashinda kila mchezo,” alisema Niyonzima.
0 COMMENTS:
Post a Comment