February 13, 2020

PAUL Nonga, nahodha wa Lipuli amesema kuwa watapambana kupata pointi tatu mbele ya Simba kwenye mchezo unaotarajiwa kuchezwa Februari,15, Uwanja wa Samora.
Nonga ni kinara wa utupiaji ndani ya Lipuli akiwa na jumla ya mabao nane na ametoa jumla ya pasi nne za mabao.
Akizungumza na Saleh Jembe, Nonga amesema kuwa kila baada ya kumaliza mchezo wamekuwa wakijipanga kwa ajili ya mchezo unaofuata hivyo watapambana mbele ya Simba.
“Ligi ni ngumu na kila timu inapambana kutafuta matokeo jambo tutakalofanya ni kujituma na kufanya kazi ndani ya uwanja kupata pointi tatu mbele ya wapinzani wetu.
“Tunatambua kwamba ni timu kubwa ila inapofika uwanjani wote ni wachezaji tumejipanga kuona tunapata matokeo, mashabiki watupe sapoti,” amesema Nonga.
Lipuli ilishinda mchezo wake wa hivi karibuni mbele ya Mtibwa Sugar kwa bao 1-0 na Simba pia ilishinda mbele ya Mtibwa Sugar mabao 3-0.

1 COMMENTS:

  1. Nawaambia Simba, Nonga kifaa hicho msikiwache weka mtego mapema

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic