Baada ya Kamati ya Uendeshaji na Usimamizi wa Ligi ya Bodi ya Ligi Kuu Tanzania (TPLB) kukutana katika kikao chake cha Februari 10, 2020. Imefikia hamuzi wa kupitia mwenendo na matukio mbalimbali ya Ligi na kufanya uamuzi ufuatao;
Mechi namba 191: Simba SC (0) vs JKT Tanzania (1)
Mwamuzi msaidizi namba mbili Kassim Mpanga amefungiwa miezi mitatu(3) kwa kosa la kushindwa kutafsiri sheria za mpira wa miguu katika mechi iliyochezwa Februari 07,2020 katika uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam. Adhabu hiyo imetolewa kwa kuzingatia Kanuni namba 39(1) ya Ligi Kuu Kuhusu Udhibiti wa Waamuzi.
Pia katika kikao hicho Kamati iliielekeza Sekretarieti kufuatilia viongozi wa vilabu na Makocha ambao hivi karibuni wamekuwa wakishutumu na kutoa matamshi yenye kukashifu na kudhalilisha viongozi,Chapa (Brand) ya Ligi na Taasisi kwa ujumla kwenye vyombo vya habari na mitandao ya kijamii kwa vipindi tofauti tofauti.
Viongozi na Makocha waliobainika ni wafuatao Kocha wa Klabu ya Namungo FC (Hitimana )-kwenye mchezo wa Simba SC na Namungo Fc, Kocha wa Klabu ya Young African Sc (Luc Aymael)-kwenye mchezo wa Yanga Sc na Lipuli, Msemaji wa Klabu ya Simba SC (Haji Manara) na Muhamasishaji wa Young African sc(Anthonio Nugaz) .
Kutokana na matamshi hayo wanapelekwa kwenye Kamati ya Nidhamu ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF).
Ligi Daraja la Pili:
Mechi namba 19C : DTB Fc 1 vs Tukuyu Stars 0
Klabu ya DTB iliomba marejeo kuhusiana na mchezo huo na Kamati imepitia na kukubaliana na utetezi wao hivyo matokeo yatabaki kama yalivyokuwa.








kama ingekuwa huyo mwamuzi amefungiwa kwa kukosea kunyoosha kibendera halafu Simba wakafunga...Hapa Saleh Jembe wangeandika kichwa cha habari muamuzi aliyekosea offside ya Farga..Walifanya hivyo kwa offside ya Kagere..Lakini kwa kuwa amefungiwa kwa kuinyima Simba bao halali basi hapa inaandikwa kafungiwa kwa kushindwa kutafsiri sheria...Salehe Jembe habari zenu huwa zimeegemea upande mmoja
ReplyDeleteHata mimi nimeshangaa huyo mwamuzi kushindwa kutafsiri sheria ipi sema hata sheria ya offside tuelewe
ReplyDeletemsishangae blog nyingi na wachambuzi wake ni wa mtaa wa pili ivo wacha tulishwe matango pori. Ndio maana Haji hawapepesei macho.wanafikili ni enzi ya Ujima kuwa wanaosoma hawajui kitu.Hata siku moja uambiwi mtaa wa pili wamefaidika na offside. izo ndio standards za wachambuzi wetu. Ndio maana hutasikia mtaa wa pili wakiwa kwenye mashindano ya kimataifa wanaitwa "underdogs" wenye mpira wanaita timu zisizo kuwa na historia ya kushinda "outsiders" na hao wachambuzi wanajua ilo lakin kwa kuwa ni Simba wanaipa neno la kejeli. Na hao hao ndio wanao sema sana kuwa mpira wa nchi hii hauwezi kukua!!
ReplyDelete