UBORA anaoendelea kuuonyesha mshambuliaji wa Simba, Meddie Kagere, katika kupachika mabao umefunika uwezo wa klabu za Singida United na Ndanda FC.
Kagere ndiye kinara wa ufungaji mabao katika Ligi Kuu Bara, ambapo baada ya kufunga bao moja juzi dhidi ya Namungo FC, anakuwa amefikisha mabao 12, idadi ambayo imeshindwa kufikiwa na klabu hizo mbili.
Ndanda wamefunga mabao sita pekee katika michezo 16, waliyocheza ikiwa ni nusu ya yale aliyofunga Kagere, huku wakikusanya pointi tisa, wakifungwa mechi tisa, sare sita na kushinda mchezo mmoja, wakiwa wanaburuza mkia kwenye msimamo.
Wakati kwa upande wa Singida United, wenyewe wamefunga mabao nane katika michezo 17 waliyocheza, wakivuna pointi 10, baada ya kushinda michezo miwili, sare katika michezo minne na kupoteza mechi 11, wakiwa wanashika nafasi ya 19 katika msimamo wa ligi hiyo.
“Siku zote nimekuwa nikipambana kuisaidia timu yangu kupata matokeo, sipendi kushindana na mtu, huwa najitahidi kutimiza malengo yangu," amesema Kagere.
0 COMMENTS:
Post a Comment