February 20, 2020


KOCHA Mkuu wa Tottenham, Jose Mourinho amesema kuwa hakuwa na namna ya kuwazuia wapinzani wake RB Leipzig kutokana na wachezaji wake muhimu kusumbuliwa na majeruhi hivyo ingekuwa sawa na kwenda vitani kupigana ukiwa na bunduki isiyokuwa na risasi.

Spurs ilifungwa bao 1-0 hilo na RB Leipzig lilifungwa dakika ya 58 kupitia kwa Timo Werner lilidumu mpaka mwisho wa mchezo huo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya hatua ya 16 bora.

Mourinho amesema kuwa alikuwa na mashaka makubwa endapo wapinzani wake wangemfunga bao jingine kutokana na kuzidiwa mbinu ndani ya uwanja baada ya kuwakosa wachezaji wake ambao wanasumbuliwa na majeruhi.

Spurs iliwakosa nyota wao wawili ambao ni Son Heung-min na Harry Kane ambao ni washambuliaji tegemeo ndani ya kiksoi hicho kutokana na kusumbuliwa na majeruhi, mchezo wao wa marudio unatarajiwa kuchezwa Machi 3.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic