February 26, 2020

GARY Neville, mchezaji wa zamani wa Manchester United amesema kuwa anaamini nyota wa Liverpool, Mohamed Salah anaweza kujiunga na timu za Barcelona ama Real Madrid wakati ujao.
Neville amesema kuwa anatambua uwezo wa mshambuliaji huyo ni mkubwa na huenda mashabiki wake wengi watafurahi kumuona akipata changamoto mpya akiwa sehemu nyingini.
Salah raia wa Misri, ametupia jumla ya mabao 90 kwenye mechi 140 ambazo amecheza mpaka sasa akiwa na Liverpool ambayo alijiunga nayo mwaka 2017 na ametwaa ubingwa wa Ligi ya Mabingwa akiwa na timu hiyo.
"Sio kitu chepesi kumpata mchezaji kama Salah na niliwahi kusema miezi 18 iliyopita kuwa Salah yupo njiani kuondoka ndani ya Liverpool.
"Ninaamini itakuwa ngumu kutokana na mashabiki wake wa Liverpool kupenda kumuona pale ila wapo wengine ambao watapenda kumuona sehemu nyingine kutokana na thamani yake aliyojiwekea,".

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic