ZINEDINE Zidane, Kocha Mkuu wa Real Madrid amesema kuwa, Pep Guardiola ni miongoni mwa makocha bora anaowaheshimu kutokana na kazi zao wanazozifanya.
Real Mdardi na Manchester City zitakuwa kazini leo Uwanja wa Bernabeu kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya.
"Amekuwa bora kwenye timu nyingi ambazo amefundisha alikuwa Barcelona kisha Munich na sasa yupo na Manchester City kwa maoni yangu, yeye ni kocha bora wengine watafikiria kumtaja kocha mwingine.
"Kiukweli ninapenda kile anachokokifanya na ninapenda kazi yake kwani ananishawishi nami pia kwenye utendaji wangu wa kazi. Kwa namna ambavyo ninajifunza kwake sina hofu ya kushuka uwanjani kukutana na timu yake ama kucheza naye kwa kuwa ni mtu ninayemkubali,"amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment