March 24, 2020

ASTON Villa, klabu anayokipiga Mbwana Samatta nahodha wa Tanzania ndani ya Ligi Kuu England imejikusanyia pointi 25 baada ya kucheza mechi 28.

Villa imefunga jumla ya mabao 34 ambapo moja kati ya hayo Samatta naye alipachika bao moja pia.

Imeshinda mechi 4 na kupoteza mechi 16 na kulazimisha sare 7 ndani ya Ligi Kuu England ipo nafasi ya 19 ina kazi kubwa ya kufanya kwenye mechi zake zlizobaki ili kujinasua kutoka hatari ya kushuka daraja.


Samatta alijiunga na Klabu ya Aston Villa akitokea timu ya KRC Genk ambapo mpaka sasa amecheza mechi nne za Ligi Kuu England. 

Kwa sasa ligi ya England imesimama na inatarajiwa kurejea Aprili 30 kutokana na kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.

1 COMMENTS:

  1. Data zako ni zauongo brother tena hata huwezi kuangalia ukarekebisha dah pole sana.wameshinda game 4 sawa na alama 12 wakasuluhu game 7 sawa na alama 7 kwahyo jumla wana alama 19,sasa mbina unatuambia wana alama 25??

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic