ASTON Villa na Brighton zote timu za England zimechangia zaidi ya milo 1300 kama misaada kwa wasio na makazi baada ya mechi za wiki hii kuahirishwa.
Ijumaa ya wiki hii Ligi kuu ya England imesitishwa hadi Aprili 3 kutokana na kuenea kwa virusi vya corona.
Hivyo Vyakula vilivyokuwa tayari vimeandaliwa kuuzwa kwa mashabiki vimetolewa kama msaada kwa wasio na makazi na wenye uhitaji. Hii ni kuhakikisha kuwa hakitaharibika.
Klabu ya Brighton Albion pia imejitolea kuwalipa wafanyakazi ambao hawawezi kufika kazini kwa sababu ya hofu juu ya ugonjwa wa Corona, pamoja na wafanyakazi wa kawaida zaidi ya 600 ambao wanafanya kazi kwenye klabu siku ya mechi.
Aston Villa yupo nyota wa kitanzania, Mbwana Samatta ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya Tanzania.
0 COMMENTS:
Post a Comment