UONGOZI wa
Simba umesema kuwa ushindi wa mabao 8-0 walioupata mbele ya Singida United
umewapa nguvu wachezaji na wamekubaliana kuendelea kupata ushindi kwenye mechi
zao zinazofuata ili kufikia melengo waliyojiwekea.
Ushindi huo
ni mkubwa kutokea kwenye mechi zote zilichezwa ndani ya Ligi Kuu Bara msimu wa
2019/20 na uliibuka na hat trick ya kwanza kwa mchezaji wa Simba Meddie Kagere.
Akizungumza na Saleh Jembe, Katibu Mkuu wa Simba
Dr, Arnold Kashembe amesema kuwa wamezungumza na wachezaji ili kuona wanaendeleza
pale walipoishia kwa kupata ushindi mkubwa ili waendelee kufukuzia malengo
waliyojiweka.
“Ligi kwa
sasa imesimama kwa baadhi ya timu kutokana na wachezaji wa timu nyingi
kujiunga na kambi ya timu ya Taifa lakini haina maana kwamba hatuna jambo la
kufanya timu inaendelea na mazoezi na ushindi wa mabao 8-0 tulioupata tunahitaji
uwe mwendelezo kwa mechi zetu zinazofuata.
“Mchezo wetu
unaofuata utakuwa dhidi ya Ruvu Shooting lakini bado haujapangiwa tarehe,
tukitambua itakuwa lini hapo tutajua mpango wa kuanza kuiwinda rasmi ili kupata
pointi tatu ila kwa sasa tunaendelea na mazoezi,” amesema Kashembe.
Mchezo wao
wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru, Simba ilishinda mabao 3-0 na kusepa na pointi tatu mbele ya Ruvu.
0 COMMENTS:
Post a Comment