March 24, 2020


IMEELEZWA kuwa nyota wa Simba, Clatous Chama amegoma kuongeza kandarasi ndani ya klabu yake hiyo kwa ajili ya kuendelea kuitumikia timu hiyo.

Uongozi wa Simba ulifanya mazungumzo na nyota huyo ambaye mkataba wake unatarajia kumeguka mwishoni mwa msimu huu wa Ligi Kuu Bara.

Taarifa zinaeleza kuwa kiungo huyo aligoma kuongeza kandarasi na kuwataka mabosi wa Simba wasubiri kwanza mpaka pale mkataba utakapomeguka jambo lililoibua wasiwasi kwa viongozi hao kuhofia kuzidiwa ujanja na klabu nyingine.

Kwa sasa Chama hayupo Bongo yupo zake nchini Zambia baada ya Ligi Kuu Bara kusimamishwa kwa muda ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona. 


"Kuna uwezekano mkubwa Chama kuhama klabu ya Simba mwishoni mwa msimu hii ni baada ya kugomea mkataba mpya aliopewa kwa ajili ya kusaini baada ya ule wa miaka miwili kumalizika mwishoni mwa msimu huu. 

"Chama ameomba kusaini mkataba huo baada ya ligi kumalizika, kitu ambacho viongozi hawataki kuskia Kwa hofu kuwa nyota huyo anaweza kuibukia klabu nyingine," kilieleza chanzo.

Katibu Mkuu wa Simba, Dr.Arnold Kashembe amesema kuwa hilo ni suala la kiutawala hawezi kulizungumzia kwa kuwa muda wa usajili bado.

7 COMMENTS:

  1. Democratic country under the democratic zone of sports,you can not force the water to go up the hill,simple mind will simplify tough challenges and become so smooth like bread on the cup of tea,"waambie waliwale waje wale waliwao"the time is this why do they dont come fast??let me satirized,only the FOOLS will understand.

    ReplyDelete
  2. Ninachojua if you recognize and understand the statements above,automatically you are not a fool,you are more than intellectual.

    ReplyDelete
  3. Endeleeni tu kutafuta habari za kizushi na kuzifanya habari kamili ili muuze magazeti.

    ReplyDelete
  4. Hamna kazi ingine zaidi ya kutengeneza uwongo na fitina zenu ili muuze habari za kizushi na uwongo mmechemka

    ReplyDelete
  5. kweli huyu jamaa sijui habari zake anaokota wapi aisee 28/6/2019 Cretus Chota Chama alisaini mkataba mpya simba sport club na atakuepo simba mpaka 2023

    ReplyDelete
  6. Dada hivi ligi zote duniani zimesimama hakuna habari za kuuza magazeti zaidi ya uzushi

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic