ARSTICA Cioaba, Kocha Mkuu wa Azam FC amekasirishwa na mabao 37 yaliyofungwa na wachezaji wake ndani ya Ligi Kuu Bara na kuwataka washambuliaji wake wongeze umakini wakiwa ndani ya 18.
Safu ya ushambuliaji ya Azam, FC inaongozwa na Obrey Chirwa mwenye mabao nane na Idd Seleman ‘Naldo’ mwenye mabao matano imepotezwa na ile ya Simba inayoongozwa na Meddie Kagere ikiwa na jumla ya mabao 63.
Cioaba alisema kuwa washambuliaji wake wanapoteza nafasi nyingi wakiwa ndani ya 18 jambo linalowafanya washinde kwa mabao machache kwenye mechi zao za ligi.
Akizungumzia hilo, Mtendaji Mkuu wa Azam FC, Abdulkarim Amin alisema kuwa wanafanyia kazi masuala ya kiufundi ambayo wanaamini yatakwishwa na timu itakuwa ikipata matokeo mazuri.
“Tupo kwenye maboresho ya kikosi chetu na kuna mapungufu ambayo mwalimu anayatambua hayo tutayafanyia kazi ili kuongeza nguvu ya ushindani, wachezaji wengi ambao tumeona wanatufaa tumewaongezea mkataba huo ni mwanzo,” alisema Amin.
0 COMMENTS:
Post a Comment