GADIEL
Michael, beki wa timu ya Simba amesema kuwa bado ana nafasi ya kufanya makubwa
ndani ya Simba kutokana na uwezo alionao.
Gadiel
alisajiliwa na Simba kwenye dirisha kubwa la msimu wa 2019/20 akitokea Yanga
ambapo akiwa Simba amecheza mechi nane ambazo ni sawa na dakika 720 hku
akikosekana kwenye mechi 20 ambazo ni sawa na dakika 1,800.
Vita yake
kubwa ndani ya Simba ni dhidi ya Mohamed Hussein,’ Tshabalala’, kwa wakati huu
wa mapumziko kwa ajili ya kuzuia maambukizi ya Virusi vya Corona amesema
amepewa program na Kocha Mkuu Sven Vanderbroek jambo analoamini litamrejesha
kwenye ubora.
"Sina tatizo na uwezo wangu na ninajua kwamba bado nafasi ipo ya kurejea kwenye ubora, kikubwa ni kujituma na kuendelea kufanya mazoezi, ishu ya namba ipo chini ya mwalimu ila bado ninafanya mazoezi kwa sasa kujiweka fiti," amesema.
Simba
imejikusanyia pointi 71 kibindoni na inaongoza Ligi Kuu Bara na imefunga mabao
63.
Mungu atakusaidia
ReplyDeleteHamna kitu apo wamekuaribia mpira utakaa benchi Hadi mkataba uishe na wanakubwaga
ReplyDeleteNan kamharibu mwenyewe au coach, maana kama ni mzur si atapangwa?
DeleteHuyu inabidi ajaribu kucheza namba nyingine kwa sababu Tshabalala yupo kwenye ubora zaidi na anamshawishi kocha kuendelea kumpanga.
ReplyDelete