WILLIAM Luccian,'Gallas' amesema kuwa kitakachowaumiza wachezaji wengi ni kuanza kutafuta upya nguvu ya kurejea kwenye ubora wao kwenye ligi mpaka pale watakapocheza mechi tatu ama nne kutokana na kutocheza kwa muda mrefu.
Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajiwa kurejea baada ya mwezi mmoja kupita na itategemea kutengamaa kwa hali ya maambukizi ya Virusi vya Corona.
Beki huyo mwenye umbo la kawaida ukikutana naye lakini anayofanya uwanjani ni makubwa ikiwa ni pamoja na kupambana na wachezaji wenye miili mikubwa kama David Molinga wa Yanga na Meddie Kagere wa Simba.
Akizungumza na Saleh Jembe, Gallas anayekipiga ndani ya Polisi Tanzania iliyo chini ya Kocha Mkuu, Malale Hamsini amesema kuwa kutopata mechi za ushindani kwa mchezaji kunamrudisha mwanzo kabisa.
"Mchezaji akiwa nyumbani na hafanyi mazoezi ule morali unapungua na pale atakaporudi uwanjani ni sawa na kwamba anakwenda kuanza mambo upya na kasi yake itarejea baada ya kucheza mechi tatu ama nne hivi.
"Afya ni muhimu kuliko hata morali ya wachezaji kwa sasa kwani hili lililotokea ni janga letu sote muhimu kuomba dua ili hali ilejee kama zamani," amesema.
Ligi Kuu Bara kwa sasa imesimama kutokana na kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona.
0 COMMENTS:
Post a Comment