BERNARD Morrison, kiungo mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa watani zake wa jadi Simba washukuru kwa kuwa aliumia angewaliza kwa mabao mengi siku ya Machi 8 Uwanja wa Taifa.
Morrison aliyepachika bao la ushindi wakati Yanga ikisepa na pointi tatu mbele ya Simba dk ya 44 kwa mpira wa adhabu alitoka kipindi cha pili na nafasi yake ilichukuliwa na Patrick Sibomana dk ya 56.
"Simba washukuru kuwa nilitoka mapema sikumaliza dk zote 90, sikuwa na hofu na dabi kutokana na uzoefu wangu nilionao kwenye mechi kubwa na ngumu endapo ningemaliza dk zote ningewafunga mengi siku hiyo," amesema.
Yanga imefikisha pointi 50 ikiwa nafasi ya tatu imecheza mechi 26 kwenye Ligi Kuu Bara, mchezo wake unaofuata ni dhidi ya Namungo, Uwanja wa Majaliwa siku ya Jumapili.

Ha ha ha ha tena nafikiri ni bora ulivyotoka maana ulikua umeshakata moto ungeweza kusababisha goli lirudi wewe.
ReplyDeleteAmesema kweli,Simba AKA mbeleko fc wanapaswa washukuru sana kuumia kwake mana angewaliza tu kwa bao lingine,Simba hamna kitu mabao yao mngi wameyapata kwa kubebwa tu,mechi wasipobebwa wanachapwa,mechi walioshinda kialali ni moja tu mechi ya Singida mana waliikuta imeshajifia zamani
ReplyDeleteKwenye ligi anagori ngapi mpaka Sasa
ReplyDeleteEnter your reply...uliza hivi kwani kwa simba anamagoal mangapi uambiwe
Deleteashukulu mungu kamati ilipitisha jina lake kufunga goli mwambie simba na yanga tunazijua sisi watz
ReplyDelete