March 14, 2020


HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Namungo amesema kuwa kwa sasa kikosi chake kinajiandaa na mchezo wake wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga unaotarajiwa kuchezwa Jumapili Uwanja wa Majaliwa.

Namungo ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa na pointi 49 itamenyana na Yanga iliyo nafasi ya tatu na pointi 50 kibindoni.

Akizungumza na Saleh Jembe, Thiery amesema kuwa maandalizi yapo vizuri na wanaamini wanakutana na timu bora jambo linalowafanya nao wajiweke sawa kusaka pointi tatu.

"Tutakuwa nyumbani na tunatambua kwamba mchezo wetu utakuwa na ushindani hilo lipo wazi, tumejipanga na matumaini yetu ni kuona tunapata pointi tatu, mashabiki wajitokeze kwa wingi kutupa sapoti," amesema.

Mchezo huu unakuwa wa kwanza kwa Yanga kukutana na Namungo msimu huu kwenye Ligi Kuu Bara baada ya Namungo  kupanda Daraja msimu wa 2019/20. 

2 COMMENTS:

  1. Kila la kheri,Hakuna cha kupoteza,shida yetu Yanga ilikua kumfunga Simba na tumemfunga,hizo mechi nyengine hazina ishu mana km kombe wamepangiwa kupewa mbeleko fc,Sisi tutapambana kombe la fa

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hakuna waliopangiwa kuchukua ubingwa wa FA!!!!???

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic