DAVID Ruhago, Katibu Mkuu wa Yanga amesema kuwa suala la mgawao wa fedha kwa wachezaji wa Yanga wanapopata ushindi halipo kwenye mkataba wa wachezaji hivyo hawapaswi kulalamika.
Kwenye mechi ya Simba na Yanga iliyochezwa Machi 8, Uwanja wa Taifa na Yanga kushinda kwa bao 1-0 wadhamini wa Yanga ambao ni GSM waliahidi milioni 200 kwa wachezaji iwapo wangeshinda mchezo huo.
Habari zinaeleza kuwa wachezaji waliopewa mgao wa fedsdha ni wale waliokuwa kwenye kikosi kilichoz=cheza uwanjani na baadhi ya wachezaji ambao hawakucheza jambo lililoibua mpasuko ndani ya timu.
"Kuna haki za wachezaji, hamasa na zawadi, leo nikiamua kutoa zawadi ya chupa moja hakuna mtu atakaelalamika suala la hamasa nani amepata ni mgao lilifanyika na mtoa zawadi alitoa katika kuboresha lakini haipo katika mkataba.”
“Hilo linalotembea kwenye mitandao kuhusu nani kapewa nini ni jambo la kawaida katika namna ya kuhamasisha lakini si sehemu ya mkataba kwamba lazima upewe. Ni mambo ya kawaida na yanazungumzika," amesema.
Miongoni mwa sauti ambayo inatembea kwenye mtandao kwa sasa ni pamoja na ile inayojitambulishwa kwamba ni ya Makame (Abdulazizi) pamoja na Molinga (David) wakizungumzia mgao wa fedha.
Katibu si kiongozi bora maana hajui hata jinsi ya kulishughulikia na kushughulikia matatizo..Huwezi kujibu kirahisi vile kwa vitu srious. Atuambie mgao umekwendaje??ule mgao haukusema kwa wachezaji walioanza. Wote ni wachezaji wa Yanga..ebooooo!!!!
ReplyDelete