ODION Ighalo nyota mpya wa Manchester United amezidi kuimarika ndani ya kikosi hicho baada ya kuonyesha kiwango bora kwenye mchezo wa Europa League wakati wakiwambamiza wapinzani wao LASK mabao 5-0.
Mchezo huo uliochezwa bila mashabiki kutokana na mlipuko wa Corona ulioanza mwezi Januari, mchezo huo ulikuwa na ushindani mkubwa huku Ighalo akifunga moja ya bao kwenye ushindi huo na kufikisha jumla ya mabao manne tangu nyota huyo raia wa Nigeria atue ndani ya kikosi hicho akitokea Klabu ya Shanghai Greenland Shenhua na anakipiga ndani ya United kwa mkopo.
Bao la Ighalo ambalo lilikuwa la ufunguzi dk 28 lilifuatiwa na bao la Daniel James dk 58, Juan Mata dk 82 huku mengine mawili yakifungwa dk za usiku na Mason Greenwood dk 90+1, Andreas Pereira dk 90+5.
Kocha Mkuu wa Manchester United, Ole Gunnar Solskjaer amesema kuwa miguso ya Ighalo ni yenye ubora na anaamini atakuja kuwa bora hapo baadaye.
"Miguso yake ni bora na niliona akifanya miguso mitatu kabla ya ule wa nne kuachia shuti ambalo ilikuwa ngumu kulizuia, nina amini atakuja kuwa bora kwani alikuwa akijitengenezea nafasi na ameitumia,".
0 COMMENTS:
Post a Comment