March 25, 2020


KOCHA Msaidizi wa Simba FC, Selemani Matola amesema kuwa makocha wengi wanaozinoa klabu za Ligi Kuu Tanzania Bara, wanaishi kwa presha kwa kuwa hawana uhakika wa kuzipa mafanikio timu zao. 

Matola amesema hata yeye wakati anainoa timu ya Polisi Tanzania kabla ya kutua Simba, alikuwa anakumbana na hali kama hiyo kwa sababu timu nyingi za chini hazina uhakika wa kushinda michezo miwili mfululizo.


Matola amsema presha hiyo inaongezeka kwa sasa kutokana na timu nyngi kushuka daraja msimu huu.

"Msimu huu timu nyingi zinashuka daraja ambapo moja kwa moja zitashuka nne na nyingine mbili zitacheza playoff sasa hali hiyo inafanya kila kocha kuwa na presha kuona namna gani timu yake itafanya vizuri,"

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic