GADIEL Michael Mbaga alitua Simba kama sahihisho la Mohammed Hussein Zimbwe kwa maana ya kuwa akionekana ni bora kwa mambo kadhaa.
Wakati anatua Simba, Zimbwe amekuwa bora zaidi, kwa sasa ni namba tatu kwa kiwango bora na anafanya vizuri.
Maana yake, Gadiel analazimika kuanza kupigania namba upya licha ya kwamba alikuwa tegemeo Azam FC na Yanga.
Mpira ndio uko hivi, unataka mapambano kila kukicha na lazima uendelee kujituma ili upate namba na ukipata ujitume kubaki nayo.
Hawa wote ni vijana wa kitanzania wanaopambana na maisha na nia yao ni kujijenga na hakuna ubishi wote ni mabeki wazuri lakini katika maisha, mapambano ni muhimu.
Huu ni mfano mzuri wa maisha kwamba mambo mazuri yanapatikana kupitia Juhudi na Maarifa, yanatofuata yanakuwa ni nyongeza.
Ukweli ni kwamba kumchukua Gadiel awe mbadala wa Zimbwe ni uzwazwa na kama kweli kulikuwa na nia basi ilikuwa ni kukomoana. Hawa hawawezi kucheza pamoja na hivyo hakuna anayeweza kufuta makosa ya mwenzie. Ukweli ni kwamba hata timu ya Taifa bado Zimbwe alikuwa anamuweka bench Gadiel, hata hilo Simba hawakuliona? Hawa wote wana udhaifu wao, ni wazuri kushambulia ila wanasahau kujilinda. Kibaya zaidi wana maumbo ya kitz ambayo sio rafiki linapokuja suala la kiulinzi. Kama simba walitaka mbadala wa Zimbwe, walitakiwa kwenda zaidi ya hapo. Zimbwe na Gadiel ni sawa na Vitz na IST, wote sawa itategemea unataka kuwatumiaje ila ukweli mmoja hawezi kuwa mbadala wa mwingine.
ReplyDelete