MSHAMBULIAJI wa Mbao FC, Wazir Jr amesema kuwa kwa sasa anaendelea kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona huku akifanya mazoezi ya kulinda kipaji chake ili kuwa bora pale Ligi Kuu Bara itakaporejea.
Ligi Kuu Bara kwa sasa imesimama kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona ambapo Serikali kupitia kwa Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, Machi 17 alitoa tamko hilo.
Akizungumza na Saleh Jembe, Wazir amesema kuwa kwa sasa amekuwa akitumia muda mwingi kufanya mazoezi pamoja na kuchukua tahadhari ya Virusi vya Corona.
"Nipo kwa sasa ninaendelea kujiweka sawa na ninachukua tahadhari ya Virusi vya Corona kwani hali sio shwari ni lazima tujilinde ili kuwa bora.
"Mazoezi ninafanya hasa ukizingatia kwamba mimi ni mchezaji lazima nilinde kipaji changu ili ligi itakaporejea niwe bora na nizidi kufanya vizuri," amesema.
Wazir ametupia mabao saba ndani ya Ligi Kuu Bara huku timu yake ya Mbao FC ikiwa imefunga mabao 19 baada ya kucheza mechi 28 ipo nafasi ya 19 kwenye msimamo wa ligi ikiwa na pointi 22 kibindoni.

0 COMMENTS:
Post a Comment