January 5, 2020


KOCHA Mkuu wa Simba, Sven Vanderbroeck amesema kuwa ameshangaza na uwezo wa wachezaji wake kushindwa kulinda mabao ambayo waliyafunga kwenye mchezo wao dhidi ya Yanga.

Simba jana ilianza kushinda mbele ya Yanga kwenye mchezo wao wa kwanza uliochezwa uwanja wa Taifa mabao yao yalifungwa na Meddie Kagere dakika ya 42 na Deo Kanda dakika ya 47 akimalizia pasi ya Kagere, Yanga walianza kurejea mchezoni dakika ya 50 kwa kufunga bao la kwanza kupitia kwa Mapinduzi Balama kabla ya dakika ya 54 Adeyum Saleh kumchonganisha beki Mohamed Hussein aliyejifunga bao la pili mbele ya Mohamed Issa na kufanya mzani uwe sawa.

Akizungumza na Saleh Jembe, Sven amesema kuwa wachezaji wake walijisahau na kufanya mambo ambayo alishangaa kuyaona uwanjani.

"Sijui nini kiliwakuta wachezaji kwani baada ya kuongoza kwa muda walidhani wamemaliza kila kitu wakajisahau na kuruhusu mabao mawili ndani ya dakika saba, hili jambo ni baya kwangu na sijapenda kulishuhudia," amesema.

Simba inafiksha jumla ya pointi 34 ikiwa imecheza mechi 14 huku Yanga ikiwa imefikisha jumla ya pointi 25 ikiwa nafasi ya 15 na imecheza mechi 12. 

8 COMMENTS:

  1. Hao wachezaji wa tza hata uwape nini hakuna kitu mshahara mzuri kambi hotel kubwa bonasi na nk lakini hakuna kitu imeniuma sana nakushauri MO achana na hii timu yetu haina shukurani hawa wachezaji shida sana yani

    ReplyDelete
    Replies
    1. acha unafiki ww na kocha wao.
      kwan simba isifungwe na yanga ina nn ?
      maan city anafungwa na timu ndogo,sasa ndo iwe simba ?

      Delete
    2. Wewe siyo mshabiki wa Simba sc..

      Delete
  2. Kwani mie nauliza yanga kaifunga simba si droo maana yake ni hakuna mbabe wajinga walio toka droo wakaona wameshinda na wajinga pia walio ona kutoka droo na yanga kuwa wachezaji wabaya mechi ya jana ilikuwa ni uzalendo zaidi kuliko kiufundi .mechi ya watani raja wacheze wazawa ndio raha wachezaji wa kigeni hawajui ushindani wake simba ilikosea tangu mwanzo 11 yake haikuwa sawa .na kocha simba sasa atajuwa kujirekebisha kuwa na magoli 2 haijamaanisha umeshinda ni funzo limejirejea tena yanga pia iliwahi kuwa 3 bila wakiongoza mpaka kipindi cha kwanza .simba ikafanya mabadiliko ikawaingiza wachezaji 3 wazawa kipindi cha pili na matokeo yake simba ikarejesha magoli yote 3 Kesha wa yanga hakuamini kilicho tokea wakati huo yanga wanafanya mbwembwe ngasa kukalia mpira na choo tele dakika 90 simba 3 yanga 3 yanga wakaondoka wanalia na hicho ndicho kilicho wakuta simba jana kwa hivyo tusiwe tunalaumu sana mechi ya simba yanga haitabiriki kabisa unaweza ukasajili mesi pia ukafungwa

    ReplyDelete
  3. Enter your comment...eti yanga ipo nafasi ya 15 ovyooo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic