March 24, 2020

MABAO 19 ya mshambuliaji wa Simba Meddie Kagere yamewapoteza nyota tisa wa kigeni wanaokipiga ndani ya Yanga kwa sasa.

Kagere akiwa ni kinara wa utupiaji ndani ya Ligi Kuu Bara ambayo imesimamishwa kwa sasa, amefunga mabao 19 na kutoa pasi tano za mabao huku wachezaji wa kigeni wa Yanga kwa ujumla wamefunga mabao 18.

Nyota wa Yanga ambao wamesajiliwa ni pamoja na Bernard Morrison mwenye mabao matatu na ana pasi tatu za mabao, Yikpe Gnamien ana bao moja, Haruna Niyonzima ametupia bao moja huku Patrick Sibomana akitupia mabao matano na pasi tatu za mabao.

David Molinga ametupia mabao nane, Papy Tshishimbi, Lamine Moro, Erick Kabamba na kipa Farouk Shikalo hawana bao.

Simba imefunga mabao 63 ndani ya Ligi Kuu Bara kwenye mechi 28 huku Yanga ikifunga mabao 31 kwenye mechi 27.

1 COMMENTS:

  1. Acheni unazi ivi kati ya simba na yanga aliyekua amekamia mechi ni nani?wenzenu simba wamecheza mpira wa kiwango chao na ndiomana ukiacha mechi ya simba na yanga bado waliendelea kushinda mechi yao iliyofuata tena kwa magoli mengi mpaka aibu,je kilichowakuta nyinyi baada ya mechi ya watani mnakijua?na je mnajua sababu kwanini mlifungwa na tena kwakucheza chini ya kiwango?unajua kwanini mechi iliyofuata mlisuluhu?hapo ndipo utakapopata majibu yatakayopingana na hoja yako kwamba eti simba walikamia mechi,ule ni mpira wa simba yani ni kawaida ya simba kucheza kiwango kile,na walichokifanya simba nikusoma akili za yanga basi na walivyogundua wamekamiwa ndipo walipoamua kurelax kama unabisha chunguza haswa kipindi cha pili,madhara yakukamia mechi ni makubwa sana na mara nyingi yanakua ni hasara inayoigharimu timu maana wachezaji walijitoa mhanga kwakutumia nguvu za ziada hatimae mnakuja kufungwa mechi kibao kama kilichowakuta yanga,kwa mpira mliocheza na simba kama mngelikua mnacheza vile kila siku leo hii mngekua ndio mpo pale kileleni mkisubiri kutawazwa kuwa mabingwa wa VPL,lakin mnakamia mechi ya watani alafu madhara yake ndio haya,poleni sana maana mtaendelea kufungwa sana tena mpaka mtachukiana wenyewe,POVU RUKSAAAAAAAAAAA

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic