December 22, 2020



 UONGOZI wa Simba umesema kuwa kuchelewa kukamilika kwa vibali vya kiungo mkabaji mpya wa Klabu ya Simba raia wa Uganda, Taddeo Lwanga ni sababu kubwa ya nyota huyo kuchelewa kuanza majukumu yake mapya ndani ya Simba.

Lwanga alikamilisha usajili wake na kutambulishwa kujiunga na Simba, Desemba 2, mwaka huu ambapo alianza mara moja mazoezi na kikosi cha mabingwa hao watetezi, mpaka sasa hajacheza mchezo huku kukamilika kwa vibali vyake ikiwa ni kitendawili.

Akizungumzia kuhusu vibali vya Lwanga Ofisa Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amesema: "Bado tunapambana kuhakikisha tunakamilisha vibali vya kiungo wetu mkabaji, Taddeo Lwanga vinakamilika ili nyota huyo aanze kuitumikia Simba rasmi.

"Tumefikia mahali pazuri katika hilo na ni matumaini yetu kuwa hivi karibuni kila kitu kitakuwa kimekamilika," .


Nyota huyo amesaini dili la miaka miwili ndani ya Simba akiwa amepewa jezi namba nne ambayo ilikuwa inavaliwa na nyoya, Gerson Fraga.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic