MANCHESTER United na Manchester City imeripotiwa kwamba zina nafasi ya kuipata saini ya nyota raia wa Hispania, Sergio Ramos ambaye yupo ndani ya kikosi cha Real Madrid kinachohitaji kuinasa saini ya mshambuliaji Kylian Mbappe.
Beki huyo wa kati mwenye miaka 35 atakuwa mchezaji huru pale mkataba wake utakapomeguka Juni 30 na kumekuwa hakuna mrejesho wowote kuhusu kuongeza mkataba wake kutoka kwa mabosi wake wa sasa.
Ripoti zimekuwa zikieleza kuwa kumekuwa hakuna mahusiano mazuri kati ya Ramos na Rais wa Real Madrid, Florentino Perez jambo linalomaanisha kwamba ataondoka mkataba wake utakapoisha.
Sababu nyingine ni kwamba katika orodha ya wachezaji 10 ambao hawakuwa na furaha ndani ya Real Madrid na jina la Ramos pia lilikuwa ndani ya wachezaji hao na ripoti zimeeleza kuwa kutokana na janga la Corona Real Madrid inahitaji kumpa dili mshambuliaji wa PSG Mbappe.
Ramos akiwa na Real Madrid ametwaa mataji matano La Liga, manne ya Ligi ya Mabingwa Ulaya ni miongoni mwa wachezaji ambao wamefanya vizuri katika kikosi hicho.
0 COMMENTS:
Post a Comment