March 24, 2020

BEKI mkongwe ndani ya Klabu ya Simba, Erasto Nyoni amesema kuwa anaamini kuwa atajumuika na wachezaji wenzake kwenye mazoezi ya pamoja baada ya mapumziko ya mwezi mmoja kukamilika.

Nyoni alipata majeraha kwenye mchezo dhidi Yanga uliopigwa Uwanja wa Taifa Machi 8 ambapo Yanga iliibuka na ushindi wa bao 1-0.

Kwa sasa Ligi Kuu Bara imesimama kwa muda ili kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona kwa muda wa mwezi mmoja.

"Nina amini kwamba baada ya muda wa mwezi mmoja nina amini nitaungana na wenzangu kwenye mazoezi, kikubwa ni kuomba Mungu tuwe salama kwani hili janga ni letu sote," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic