SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wachezaji wake wote ni wazuri ila anashindwa kuwatumia kutokana na kushindwa kumshawishi pale wanapopata nafasi.
Miongoni mwa nyota ambao wamekuwa wakikosekana uwanjani ni pamoja na Ibrahim Ajibu, Shiza Kichuya, Said Ndemla, Yusup Mlipili,Beno Kakolanya.
Kichuya, Kakolanya na Ajibu mchezo wao wa mwisho ulikuwa ni wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Stand United huku Mlipili akiwa nje kwa muda mrefu.
Sven amesema kuwa wachezaji ambao hawatumii bado hawajamshawishi jambo ambalo linamfanya asiwatumie na kutaka wakipata nafasi wafanye kazi kubwa kumshawishi ili wapate nafasi.
"Kuna wachezaji wengi na wote ni wazuri hivyo kinachonifanya nisiwatumie wachezaji wengine ni kushindwa kwao kunishawishi, wakipata nafasi wanatakiwa kuonyesha uwezo wao wote," amesema.
Mchezaji kama hajacheza mechi yeyote lazima atavurunda kwa mechi za mwanzo hio ni kawaida sana. Confidence ya mchezaji inaongezeka kwa idadi ya mechi inazocheza. Haikuwa bahati mbaya Simba kusajili ilivyosajili na wote wanatakiwa wawe na mchango ndani ya timu. Simba wamecheza chini ya kiwango dhidi ya Yanga kutokana na match fitness ya baadhi ya wachezaji kuwa chini. Kikosi kipana maana yake wachezaji wote wana nafasi ya kucheza kama wanafanya makosa ni jukumu la kocha kumfahamisha wapi anakosea hata kwa video clips ili apate kujifunza sio kumuweka benchi na huku klabu inaingia gharama. Ligi ikiisha kuna CHAN na CAF Champions league. Wachezaji mpaka msimu ujao watakuwa hawajapumzika vya kutoa kuendana na mikikimikiki ya msimu ujao. Kocha lazima aliangalie hilo. Simba hii leo imeanza kuonesha muunganiko mzuri wa kitimu ambao ni mtaji mzuri hatutaki tena kusikia timu inaundwa upya kwa kusajili wachezaji wengi wapya ili kuridhisha mashabiki. Kama kocha ana mahitaji yake ya wachezaji basi wasizidi wawili ili wasiharibu huu muunganiko uliojengwa msimu huu. Timu haijengwi na wachezaji tu bali na muda wa hao wachezaji kucheza pamoja. La sivyo, lila msimu tutatoka katika hatua za awali za michuano ya kimataifa au kuambulia vipigo vya magoli mengi na kupata aibu.
ReplyDeleteTatizo hata Kama timu imeshinda kocha anachukua muda mrefu kufanya sub matokeo wachezaji hawapati nafasi kabisa
ReplyDeleteangewapanga mechi na Singida angeona we singida dhaifu alafu kaweka mziki mnene kweli duuu huyu kocha ne anaishi kwa mazoea
ReplyDeleteMbona kipindi cha pili wameingia lakini ni goli mbili tu zilifungwa .Hatutaki kujaribisha watu ambao hawajitaidi kuonyesha kweli wanafaa wewe ulitaka tuwaweke hao tukifungwa uanzelawama. Hatutaki masiara masiara nimemuachia chura kila mechi weka mziki mnono basi.
ReplyDeletehii ni ligi sio pre-season kwa hyo unapompanga mchezaji inabidi uwe nae uhakika wa kukupatia kitu ambacho aliyeanza hajakitimiza ni kweli unamtoa luis unaingiza ajibu? wakati huo ajibu anacheza kama na watoto wake uwanjani. Ebo ngoja simba ijihakikishie ubingwa ndo watacheza hata mechi nne zitakazobaki
ReplyDelete