March 1, 2020


SVEN Vandnbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema ataingia kwa tahadhari kubwa kuivaa KMC kutokana na ushindani uliopo ndani ya Ligi Kuu Bara.

Simba itaingia uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kushinda mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Uhuru kwa mabao 2-0. 

Sven amesema: 'Kwetu sisi kila mchezo ni muhimu kuona tunapata matokeo, ninawaheshimu wapinzani wangu na nitawafuata kwa tahadhari kubwa haina maana kwamba ukiwa bora haufungwi.

"Mashabiki wanapenda burudani na kuona timu inapata matokeo ni wakati wao kujitokeza kwa wingi kuona namna wachezaji wanavyojituma uwanjani,".

Safu ya ushambuliaji ya Simba nayoongozwa na Meddie Kagre imefunga jumla ya mabao 50 ikiwa na pointi 62 kibindoni na ipo nafasi ya kwanza

3 COMMENTS:

  1. Simba hasa wachezaji ndani ya uwanja wanatakiwa kuwa wakali na kumlinda bwana mdogo Lousi Miquissonne kutokana na ubabe na faulu za kijinga ambazo zitaelekezwa kwake kwani tulishaona kunako mechi mbili alizocheza kulikuwa na faulu kazaa za kijinga zidi yake baada ya wachezaji pinzani kushindwa kuendana na kasi yake.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Sio yeye peke yake. Kuna Kanda, Muzamiru na Madenge wote majeruhi. Faulo za kijinga.

      Delete
    2. Kuna faulo za kijinga kupitiliza na kufanya mchezaji majeruhi kukaa njee ya dimba Kwa kipindi kirefu sana na mfano dhahiri ni ya Bocco aliyeumizwa na mchezaji wa Azam.Kanda aliyofanyiwa na Juma Abdul...Rafu zilikuwa mbaya sana.unamrukiaje mchzaji mwenzako Kwa miguu miwili yaani double dachi kama sio kudhamiria?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic