IMEISHA rekodi ya timu ya Liverpool kuendelea kucheza mechi zake za Ligi Kuu England bila kufungwa baada ya jana, Februari 29 Watford kuitungua kwa mabao 3-0 kwenye Uwanja wa Vicarage Road.
Liverpool imeshindwa kuifikia rekodi iliyowekwa na Arseanl ya kucheza mechi 49 bila kupoteza ambayo waliiweka kuanzia Mei 7,2003 ikagota Oktoba 24,2004.
Kupoteza mbele ya Watford kumeipoteza jumla Liverpool iliyo chini ya Jurgen Klopp ambaye anaongoza ligi akiwa na pointi 79 kibindoni.
Rekodi ya Liverpool imeishia kwenye mechi 44 ikiwa zimepita siku 422 tangu ipoteza mchezo wake na ilichapwa mabao 2-1 mbele ya Manchester City, Januari 3,2019.
Licha ya kupoteza kwa kuchwapwa mabao 3-0 mbele ya Watford bado Liverpool inaingia kwenye rekodi ya timu tatu ambazo zimecheza mechi nyingi bila kupoteza ndani ya Ligi Kuu England.
Nyingine ambazo zilicheza mechi nyingi bila kupoteza ni pamoja na Chelsea na Arsenal.
0 COMMENTS:
Post a Comment