SIMBA kesho ina kazi mbele ya Singida United kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Taifa majira ya saa 10:00 jioni.
Wapinzani wa Simba, Singida United wapo kwenye hatari ya kushuka daraja jambo linaloongeza ugumu kwenye mechi hiyo inayotarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.
Kwenye mchezo uliopita wa mzunguko wa kwanza Simba ilishinda bao 1-0 lililofungwa na Miraj Athuman ambaye kwa sasa anasumbuliwa na majeruhi.
Simba imetoka kupoteza mchezo wake mbele ya Yanga kwa kufungwa bao 1-0 huku Singida United ikifungwa mabao 2-1 mbele ya Tanzania Prisons.
0 COMMENTS:
Post a Comment