SAID RUBEYA, SWALEHE MADJAPA, USTADH M. HASSAN,
JACKSON J. SAGONGE & VALENTINE NYALU………………..……….. Waweka
Pingamizi
DHIDI
MICHAEL RICHARD
WAMBURA……………………………..…………Muwekewa Pingamizi
MAAMUZI
Waweka Pingamizi waliotajwa hapo juu, ambao ni wanachama wa
Simba Sports Club wamemwekea pingamizi Mwekewa Pingamizi hapo juu kwa hoja
zifuatazo:
i.
Mwekewa Pingamizi aliipeleka Simba Sports Club
mahakamani katika kesi Namba 100/2010 iliyofunguliwa katika mahakama ya Hakimu
Mkazi Kisutu, Dar es salaam, Kinyume na Ibara ya 11 (1) (e), (2), 12(3), na 55 ya Katiba ya Simba Sports Club ya
Mwaka 2010.
ii.
Mwekewa Pingamizi alisimamishwa Uanachama na
Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club iliyokutana tarehe 5 Mei 2010 na barua
ya tarehe 6 Mei 2010, (Kumb. Na. SSC/MMKT/163/VOL.40/11) na hivyo basi
anapoteza haki za kuwa mwanachama wa Simba Sports Club
iii.
Mwekewa Pingamizi amekiuka Katiba ya Simba, TFF
na FIFA kwa kuipeleka Simba Sports Club Mahakamani katika kesi Namba 100/2010.
iv.
Mwekewa Pingamizi ameanza kampeni kabla ya muda
wa Kampeni
v.
Mwekewa Pingamizi amekiuka katiba ya Simba kwa
kukubali uteuzi batili kuwa mjumbe kamati ya uchaguzi.
vi.
Mwekewa pingamizi hana maadili ya Uongozi
kwasababu alikiuka maadili akiwa kiongozi wa FAT/TFF.
vii.
Mwekewa Pingamizi sio mwajibikaji.
Nakala ya mapingamizi hayo na mwaliko wa kikao cha kusikiliza
pingamizi valikabidhiwa kwa mwekewa pingamizi tarehe 23 Mei 2014. Siku ya
kusikiliza Pingamizi, tarehe 25 Mei 2014, Mwekewa pingamizi aliwasilisha mbele
ya kamati ya uchaguzi “preliminary objections” mbili kama ifuatavyo:
i.
Dhidi ya waweka pingamizi wote watano(ona
kiambatanisho “A”)
ii.
Dhidi ya Kamati ya Uchaguzi ya Simba (ona
kiambatanisho “B”)
Kabla ya kuanza kusikiliza mapingamizi ya waweka pingamizi,
kamati ilisikiliza “preliminary objections” na kutoa maamuzi kama ifuatavyo.
Mosi, “preliminary objections” dhidi ya wagombea watano (5),
kimsingi ni majibu ya pingamizi toka kwa ya wakewa pingamizi, hivyo basi, hoja
hizo zitapata fursa wakati mwekewa pingamizi anajibu hoja za waweka pingamizi.
Pili, “preliminary objections” dhidi ya kamati zinatupiliwa
mbali kwa misingi ifuatavyo;
a.
Uteuzi wa katibu wa kamati ya uchaguzi samba
sports club ulifanywa na kamati ya utendaji ambayo mweka “prelimary objections”
alihudhuria.
b.
Kamati imeamua kuazima na kutumia kanuni za
uchaguzi za TFF kwasababu Kamati ya utendaji Simba haijaandaa kanuni hizo.
c.
Unapoazima na kutumia kanuni za Mamlaka nyingine
sio lazima uzitumie kama zilivyo, una uhuru wa kufanya maboresha ili kuzingatia
hali halisi ya Simba Sports Club.
d.
Pingamizi dhidi ya Bw. Evans Aveva ni malalamiko
ya kawaida ambayo Kamati inabidi iyazingatie kwa wakati wake na sio sehemu ya
mapingamizi kwasababu muda wa pingamizi umekwisha.
e.
Kanuni hazielezi haki ya kuweka “preliminary
objections”, lakini kamati ilitumia busara kuzisikiliza.
Hivyo basi kamati ilitupilia mbali “prelimary objections” na
kusikiliza pingamizi katika mfumo wa kawaida.
Kamati, awali ya yote, ilichambua masuala ya kimaadili na
kuamua kuwa mambo hayo ya kimaadili, yapelekwe katika kamati ya maadili ya TFF
na waweka pingamizi wenyewe. Mambo ya kupelekwa kamati ya maadili ni:
i.
Mwekewa Pingamizi amekiuka katiba ya Simba kwa
kukubali uteuzi batili kuwa mjumbe kamati ya uchaguzi.
ii.
Mwekewa pingamizi hana maadili ya Uongozi kwasababu
alikiuka maadili akiwa kiongozi wa FAT/TFF.
iii.
Mwekewa Pingamizi sio mwajibikaji.
Kamati ilijadili na kuyatolea maamuzi mapingamizi yafuatayo:
i.
Mwekewa
Pingamizi ameanza kampeni kabla ya muda wa Kampeni.
Kamati ilikwisha toa adhabu ya ONYO KALI dhidi ya Mwekewa Pingamizi kuhusu
kuanza kampeni kabla ya wakati, hivyo basi hawezi kuadhibiwa mara mbili kwa
kosa ambalo ameshaadhibiwa.
ii.
Mwekewa
Pingamizi aliipeleka Simba Sports Club katika kesi Namba 100/2010
iliyofunguliwa katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, Dar es salaam, Kinyume
na Ibara ya 11 (1) (e), (2), 12(3),
na 55 ya Katiba ya Simba Sports
Club ya Mwaka 2010.
Ushahidi uliotolewa mbele ya kamati unaonyesha kuwa Mwekewa
pingamizi alifungua kesi No. 100/2010 katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu dhidi
ya Simba Sports Club katika masuala ambayo hayapaswi kwenda mahakamani. Kitendo
hicho ni ukiukwaji wa Ibara ya 11
(1) (e), (2), 12(3), na 55 ya
Katiba ya Simba ya Mwaka 2010.
iii.
Mwekewa
Pingamizi alisimamishwa Uanachama na Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club iliyokutana
tarehe 5 Mei 2010 na hivyo basi anapoteza haki za kuwa mwanachama wa Simba
Sports Club.
Kamati imepokea ushahidi na kuridhika kuwa tarehe 5 Mei 2010,
kupitia kikao halali kamati ya utendaji ya Simba Sports Club ilimsimamisha
Uanachama Mwekewa Pingamizi kwa tuhuma za kuipeleka Simba Mahakamani katika
kesi tajwa. Baada ya kusimaishwa uanachama na kamati ya utendaji kwa mujibu wa
Ibara 12(1),(2) & (3) ya katiba ya Simba mwaka 2010, jambo hilo lilipaswa
kupelekwa katika mkutano mkuu ili mkutano mkuu, utoe adhabu au utoe msamaha. Kwa mujibu wa Katiba ya Simba,
Ibara ya 55, adhabu ya kosa hilo ni kufukuzwa uanachama. Si kamati ya utendaji
wala Mwekewa Pingamizi aliyepeleka suala hili katika mkutano mkuu ili litolewe
uamuzi.
Kamati imepokea barua tatu, toka kwa Mwekewa Pingamizi,
kuhusu uanachama wake Simba Sports Club. Barua ya kwanza iliandikwa tarehe 6
Novemba 2012 toka kwa Bw. Michael Wambura kwenda kwa Mwenyekiti wa Simba. Barua
hiyo inakiri kosa la kuipeleka Simba makahamani na kuahidi kuwa hatarudia tena.
Barua ya pili toka kwa Mwenyekiti wa Simba ya tarehe 15/09/2012, Ref. No.
SSL/20/9/12, kukiri kupokea barua toka kwa Bw. Michael Wambura na kuahidi kuwa
suala hilo litafanyiwa kazi, ingawa kamati ilibaini kuwa barua ya kujibu imeandikwa
takribani miezi miwili kabla ya ile ya awali jambo ambalo haliwezekani. Barua
ya tatu ni ya tarehe 25/9/1012, kumb. SSC 28/9/12 ambayo inasema samba haina
tatizo na Bw. Michael Wambura, lakini Uhalali wa Barua hiyo unashaka kubwa sana
kiasi cha kamati kuamua ipelekwe kwenye mamlaka husika kwa hatua zaidi.
Hivyo basi kamati imejiridhisha kuwa maamuzi ya Kamati ya
utendaji ya tarehe 5 Mei 2010 ya kumsimamisha Mwekewa Pingamizi bado yanaendelea
na yana nguvu za kisheria kwasababu hakuna maamuzi yoyote ya Mkutano Mkuu
kubatilisha hatua hiyo.
Mwananchama ambaye amesimamishwa uananchama hana haki ya
kushiriki katika shughuli za simba kwa mujibu wa Ibara ya 12 (3) ya Katiba ya Simba ya Mwaka 2010
na Ibara ya 12 (3) ya Katiba ya Simba ya Mwaka 2014.
iv.
Mwekewa
Pingamizi amekiuka Katiba ya Simba, TFF na FIFA kwa kuipeleka Simba Sports Club
Mahakamani katika kesi Namba 100/2010.
Kamati inapenda kurejea maamuzi yake hapo juu katika suala ka
kwenda mahakani kwa masuala ya Soka.
Hivyo basi Muwekewa Pingamizi, Bw. Michael Richard Wambura
ameondolewa katika mchakato wa Uchaguzi, kwasababu zilizotajwa hapo juu.
Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki
ya kukata rufaa katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club
KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
ARTHUR MWAMBETA ……………………….………………..……….. Muweka Pingamizi
DHIDI
GEOFREY NYANGE
(KABURU) ……………………………..…………Muwekewa Pingamizi
MAAMUZI
Awali, kamati ilipokea mapingamizi mawili dhidi ya Muwekewa
Pingamizi toka kwa Bw. Hafidh Bashir na Bw. Arthur Mwambeta, lakini katika
mchakato wa kusikiliza, Bw. Hafidh Bashir, aliamua kuondoa pingamizi hilo. Kwa
mujibu wa maamuzi hayo tuna Muweka Pingamizi mmoja, tajwa hapo juu. Hoja za
Muweka Pingamizi ni Kama ifuatavyo:
i.
Muwekewa Pingamizi, akiwa sehemu ya Kamati ya
Utendaji ya Simba kati ya Mwaka 2010-2013 alishindwa kuwasilisha Audited
Accounts kwenye Mkutano Mkuu wa Simba, kwa mujibu wa ibara ya 19 (6), (7), 30
(1) (f) na 33 (5) ya katiba ya Simba ya Mwaka 2010.
ii.
Muwekewa Pingamizi, akiwa sehemu ya Kamati ya
Utendaji ya Simba kati ya Mwaka 2010-2013 alishindwa kujaza nafasi ya Mjumbe wa
kamati ya Utendaji (Mwanamke) iliyowazi kwa mujibu wa Ibara ya 28(1)(c) na 29
(3) ya Katiba ya Simba ya Mwaka 2010.
iii.
Muwekewa Pingamizi, akiwa sehemu ya Kamati ya
Muda ya Simba Sports Club ya Mwaka 2005, aliuza gari la Simba Sports Club
kinyume na maagizo ya Baraza la Wazee na Ibara ya 11(1) (b) na (c) na Ibara ya
6 (1) (iii) ya Simba.
Kamati ilisikiliza pande zote mbili na kuchambua ushahidi
ulioletwa mbele yake na hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:
Hoja zote tatu za pingamizi hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya
kamati ya utendaji ya Simba Sports Club na Kamati ya Muda ya Simba ya Mwaka
2005. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea binafsi. Kamati ya Uchaguzi haina
mamlaka ya kuijadili na kuitolea maamuzi dhidi ya kamati ya utendaji kwasababu
zifuatazo.
Mosi, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha
juu kuliko kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea,
hivyo ipo nje ya Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu, hakuna Ushahidi wowote dhidi ya Muwekewa Pingamizi binafsi
na kama Ungekuwepo, basi suala hilo lingefikishwa katika kamati husika na sio
kamati ya uchaguzi.
Hivyo basi Pingamizi, dhidi ya Muwekewa Pingamizi Bw. Geofrey
Nyange (Kaburu) limetupiliwa Mbali.
Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki
ya kukata rufaa katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club
KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
SAID ALI MANERO ………………………………….………………..……….. Muweka Pingamizi
DHIDI
EVANS ELIEZA
AVEVA ………….……………………………..…………Muwekewa Pingamizi
MAAMUZI
Kamati ilipokea mapingamizi dhidi ya Muwekewa Pingamizi, toka kwa Muweka Pingamizi hapo
juu. Hoja za Muweka Pingamizi ni Kama ifuatavyo:
i.
Muwekewa Pingamizi, aliwahi kugombea uchaguzi wa
DRFA mwaka 2013 kwa jina la Evans Aveva lakini katika vyeti vyake anatumia jina
la Evans Eliyeza, hivyo anaweza kuwa mtu tofauti, elimu ikwa haikidhi matakwa
ya Katiba na uraia wake kutiliwa shaka, hivyo kuiuka ibara ya 26 (1) (2) ya
Katiba ya Simba ya Mwaka 2010.
ii.
Muwekewa Pingamizi, akiwa sehemu ya Kamati ya
Muda ya Simba Sports Club ya Mwaka 2005, aliuza gari la Simba Sports Club
kinyume na maagizo ya Baraza la Wazee na Ibara ya 11(1) (b) na (c) na Ibara ya
6 (1) (iii) ya Simba.
Kamati ilisikiliza pande zote mbili na kuchambua ushahidi
ulioletwa mbele yake na hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:
Hati ya kusafiria ya Muwekewa Pingamizi namba AB 047458
iliyotolewa tarehe 26/08/2006 inamajina: Evans Elieza Aveva, hivyo hakuna utata
wowote dhidi ya jina la mgombea. Muweka Pingamizi ameshindwa kuleta Ushahidi
wowote kuhusu mashaka yake katika elimu, uanachama au uraia wa muwekewa
pingamizi, hivyo basi hoja yake ya awali katika pingamizi hili inakosa miguu ya
kikanuni na kutupiliwa mbali.
Hoja ya pili ya pingamizi hapo juu inahusu tuhuma dhidi ya
Kamati ya Muda ya Simba ya Mwaka 2005. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea
binafsi. Kamati ya Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kutoa maamuzi dhidi
ya kamati ya muda ya Simba ya Mwaka 2005 kwasababu zifuatazo.
Mosi, Kamati ya Muda ya Simba ya Mwaka 2005, ambayo hivi sasa
haipo, sio Mgombea, hivyo ipo nje ya Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Pili, hakuna Ushahidi wowote dhidi ya Muwekewa Pingamizi
Binafsi na kama Ungekuwepo, basi suala hilo lingefikishwa katika kamati husika
na sio kamati ya uchaguzi.
Hivyo basi Pingamizi, dhidi ya Muwekewa Pingamizi Bw. Evans
Elieza Aveva limetupiliwa Mbali.
Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki
ya kukata rufaa katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club
KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
MWINYI SHARIFF DOSSI……………………….………………..……….. Muweka Pingamizi
DHIDI
SWEDI MKWABI,
JOSEPH ITAN’GARE (KINESI)
SAIDI PAMBA,
IBRAHIM MASOUD &
DANIEL MANEMBE
………………………………………………..…………Muwekewa Pingamizi
MAAMUZI
Kamati ilipokea pingamizi dhidi ya Wawekewa Pingamizi toka
kwa Muweka Pingamizi tajwa hapo juu. Hoja za Muweka Pingamizi ni Kama
ifuatavyo:
i.
Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya
Utendaji ya Simba walifanya maamuzi ya kumpindua Mwenyekiti wa Simba Sports
Club kinyume na ibara ya 33 (3) (a) (b) (c) na (d) ya katiba ya Simba ya Mwaka
2010.
ii.
Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya
Utendaji ya Simba walishindwa kujaza nafasi zilizowazi ndani ya siku 90 kwa
mujibu wa Ibara ya 28(1)(c) na 29 (3) ya Katiba ya Simba ya Mwaka 2010.
Muweka Pingamizi hakutokea bila sababu yoyote, hata hivyo, Kamati
ilisikiliza utetezi wa wawekewa pingamizi na kuchambua ushahidi ulioletwa mbele
yake na hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:
Hoja zote tatu za pingamizi hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya
kamati ya utendaji ya Simba Sports Club. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya
mgombea binafsi. Kamati ya Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kutoa maamuzi
dhidi ya kamati ya utendaji kwasababu zifuatazo.
Mosi, Kamati ya Utandaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha
juu kuliko kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea,
hivyo ipo nje ya Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu, Suala hilo linapaswa kupelekwa katika kamati husika ya
maadili na sio kamati ya uchaguzi.
Hivyo basi Pingamizi, dhidi ya wawekewa Pingamizi wote hapo
juu; SWEDI MKWABI, JOSEPH ITAN’GARE (KINESI), SAIDI PAMBA, IBRAHIM MASOUD &
DANIEL MANEMBE limetupiliwa Mbali.
Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki
ya kukata rufaa katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club
KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
JAMHURI MUSSA KIHWELO……………………….………………..……….. Muweka
Pingamizi
DHIDI
SWEDI MKWABI,
JOSEPH ITAN’GARE (KINESI)
SAIDI PAMBA,
IBRAHIM MASOUD &
DANIEL MANEMBE
………………………………………………..…………Muwekewa Pingamizi
MAAMUZI
Kamati ilipokea pingamizi dhidi ya Wawekewa Pingamizi toka
kwa Muweka Pingamizi tajwa hapo juu. Hoja za Muweka Pingamizi ni kama ifuatavyo:
i.
Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya
Utendaji ya Simba walifanya kikao haramu kinyume na ibara ya 33 (4) ya katiba
ya Simba ya Mwaka 2010 na kufanya mapinduzi dhidi ya Mwenyekiti.
ii.
Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya
Utendaji ya Simba walipitisha maamuzi batili ya kuwafukuza walimu wa mpira bila
malipo na mamlaka hivyo kusababisha usumbufu mkubwa hadi leo.
Muweka Pingamizi alitoa maelezo yake na wawekewa pingamizi
walijibu hoja hizo. Kamati ilisikiliza hoja na kuchambua ushahidi ulioletwa
mbele yake na hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:
Hoja za
pingamizi hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya kamati ya utendaji ya Simba Sports
Club. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya mgombea binafsi. Kamati ya Uchaguzi haina
mamlaka ya kuijadili na kuitolea maamuzi dhidi ya kamati ya utendaji kwasababu
zifuatazo.
Mosi, Kamati ya Utandaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha
juu kuliko kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea,
hivyo ipo nje ya Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu, Suala hilo linapaswa kupelekwa katika kamati husika ya
maadili na sio kamati ya uchaguzi.
Aidha kuhusu hoja ya Kufukuzwa Walimu wa mpira, kamati inamshauri
muweka pingamizi apeleke shauri hilo katika Kamati ya Sheria ya TFF au Mahakama
ya kazi kwasababu ni suala la mwajiri na mwajiriwa.
Hivyo basi Pingamizi, dhidi ya wawekewa Pingamizi wote hapo
juu; SWEDI MKWABI, JOSEPH ITAN’GARE (KINESI), SAIDI PAMBA, IBRAHIM MASOUD &
DANIEL MANEMBE limetupiliwa Mbali na yale yanayohusu maadili
yaenda katika kamati husika.
Endapo upande wowote haujaridhika na maamuzi hayo, una haki
ya kukata rufaa katika Kamati ya Rufaa ya Uchaguzi ya TFF.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club
KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
ARTHUR MWAMBETA ……………………….………………..……….. Muweka Pingamizi
DHIDI
SWEDI
MKWABI…………………………………………………………Muwekewa Pingamizi
MAAMUZI
Muweka Pingamizi aliondoa pingamizi lake. Hivyo kamati
haikusikiliza pingamizi hilo.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club
KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
LUKA NGWAKO MBAPILA……………………….………………..………..} Waweka Pingamizi
OMAR JUMA MUNGA …………………………………………………………}
SALIM R. SIMBA ………………………………………………………………...}
ABDALLAH MKOVA ……………………………………………………………}
DHIDI
SWEDI
MKWABI…………………………………………………………Muwekewa Pingamizi
MAAMUZI
Waweka Pingamizi wote walileta hoja zifuatazo.
i.
Wawekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya
Utendaji ya Simba walishindwa kujaza nafasi zilizowazi ndani ya siku 90 kwa
mujibu wa Ibara ya 28(1)(c) na 29 (3) ya Katiba ya Simba ya Mwaka 2010.
ii.
Taarifa za mahesabu kwenye mkutano mkuu
ziliwasilishwa kwa lugha ya kiingereza hivyo kumnyima haki ya kujua mapato ya
klabu kwa miaka minne.
Waweka Pingamizi hawakutokea bila sababu yoyote, hata hivyo,
Kamati ilisikiliza utetezi wa wawekewa pingamizi na kuchambua ushahidi
ulioletwa mbele yake na hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:
Hoja zote tatu za pingamizi hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya
kamati ya utendaji ya Simba Sports Club. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya
mgombea binafsi. Kamati ya Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kuitolea
maamuzi dhidi ya kamati ya utendaji kwasababu zifuatazo.
Mosi, Kamati ya Utandaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha
juu kuliko kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea,
hivyo ipo nje ya Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu, Suala hilo linapaswa kupelekwa katika kamati husika ya
maadili na sio kamati ya uchaguzi.
Hivyo basi pingamizi linatupiliwa mbali.
Kwakuwa hawakuja kutetea pingamizi lao hawana haki ya kukata
rufaa.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club
KAMATI YA UCHAGUZI SIMBA SPORTS CLUB
MWINYI SHARIFF DOSSI……………………….………………..………..} Waweka
Pingamizi
SWALEHE MADJAPA ……………………………………………………….}
DHIDI
KARAHA HASSAN
CHANO (ALMAS)………………………………………Muwekewa Pingamizi
MAAMUZI
Waweka Pingamizi wote walileta hoja zifuatazo.
i.
Muwekewa Pingamizi, wakiwa sehemu ya Kamati ya
Utendaji ya Simba (Mhasibu Msaidizi) hakuleta taarifa za fedha katika Mkutano
Mkuu ambayo ilisababisha kuondolewa katika uchaguzi wa 2010 baada ya kuwekewa
pingamizi na Asha Kigundula na hajawahi kusamehewa na mkutano mkuu wowote.
Waweka Pingamizi hakutokea bila sababu yoyote, hata hivyo,
Kamati ilisikiliza utetezi wa wawekewa pingamizi na kuchambua ushahidi
ulioletwa mbele yake na hatimaye kutoa maamuzi yafuatayo:
Hoja zote tatu za pingamizi hapo juu zinahusu tuhuma dhidi ya
kamati ya utendaji ya Simba Sports Club. Hakuna Ushahidi wowote dhidi ya
mgombea binafsi. Kamati ya Uchaguzi haina mamlaka ya kuijadili na kuitolea
maamuzi dhidi ya kamati ya utendaji kwasababu zifuatazo.
Mosi, Kamati ya Utandaji ya Simba Sports Club ni Chombo cha
juu kuliko kamati ya Uchaguzi ya Simba Sports Club.
Pili, Kamati ya Utendaji ya Simba Sports Club sio Mgombea,
hivyo ipo nje ya Mamlaka ya Kamati ya uchaguzi.
Tatu, Suala hilo linapaswa kupelekwa katika kamati husika ya
maadili na sio kamati ya uchaguzi.
Hivyo basi pingamizi linatupiliwa mbali.
Kwakuwa hawakuja kutetea pingamizi lao hawana haki ya kukata
rufaa.
Imetolewa tarehe 26 Mei 2014.
………………………………………………….
Dk. Damas Daniel Ndumbaro (PhD)
Mwenyekiti
Kamati ya Uchaguzi Simba Sports Club
0 COMMENTS:
Post a Comment