March 24, 2020


NADIR Haroub, 'Cannavaro', Meneja wa timu ya Taifa ya Tanzania amewapa darasa wachezaji wanaokipiga Ligi Kuu Bara kuacha kubweteka kipindi hiki ambapo ligi imesimama kutokana na kuenea kwa Virusi vya Corona.

Cannavaro amewataka wachezaji kujikita kufanya mazoezi binafsi ili kulinda viwango vyao na sio kukaa kwa kuwa wamepewa mapumziko ya siku 30.


 "Wachezaji wanatakiwa wafahamu hili janga ni la dunia hivyo lazima wajiongeze kipindi hiki cha mapumziko na kufanya mazoezi binafsi ambayo yatalinda vipaji vyao.

"Jambo la msingi kwa wachezaji ni kulinda vipaji vyao endapo watatumia muda mwingi kupumzika itawaondoa kwenye reli na kuwafanya washindwe kuleta ushindani pale ligi itakapoanza," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic