March 26, 2020


IMEELEZWA kuwa baadhi ya wachezaji wa Singida United wamepania kutimka jumlajumla ndani ya kikosi hicho baada ya siku 30 kukamilika.

Ligi Kuu Bara kwa sasa imesimama kutokana na kupisha maambukizi ya Virusi vya Corona jambo lililosababisha timu nyingi kuvunja kambi.

Habari kutoka ndani ya Singida United zinaeleza kuwa wachezaji wa Singida United waliosepa kwa ajili ya mapumziko hayo wamepanga kutorejea ndani ya klabu hiyo kutokana na kudai stahiki zao.

"Wachezaji wamepanga kutorejea ndani ya kikosi cha Singida United kutokana na kutolipwa stahiki zao hivyo wameamua kutumia muda huu kuondoka kikosini moja kwa moja," ilieleza taaarifa hiyo.

Singida United ipo nafasi ya 20 ikiwa imecheza mechi 29 imeshinda mechi tatu na sare sita ikiwa na pointi 15.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic