HARUNA Niyonzima, Kiungo mshambuliaji wa Yanga amemshauri kiungo wa Simba Said Ndemla kutafuta changamoto mpya ili apate nafasi ya kucheza.
Ndemla kwa sasa ndani ya Simba iliyo chini ya Sven Vandenbroeck amekuwa hana nafasi ya kucheza kwani kwenye mechi 18 ambazo kocha huyo amesimamia amecheza mechi moja.
Mechi hiyo ilikuwa Uwanja wa Taifa ambapo Simba ilicheza na Ndanda FC na Simba ilishinda mabao 2-0.
Niyonzima amesema:"Ndemla ni kiungo mzuri na ana uwezo mkubwa wa kucheza tatizo ni kwamba anakosa namba kutokana na ushindani uliopo, wakati wake ni sasa wa kutafuta changamoto mpya ili alinde kipaji chake,".
Hivi niyonzima ndio yanga jamani
ReplyDeleteWaandishi hawa hawajui wajibu wao kwa kweli. Hatuna hakusema kuwa ametumwa na Yanga kuzungumza Ndemla aondoke, bali alitoa maoni yake ili Ndemla alinde na kuendeleza kipaji chake kupitia kwenye timu ambayo itampa nafasi ya kucheza kwani ni mchezaji mzuri
DeleteNiyomiza anafaa kuwa mtetezi wa haki za binaadamu lakini pia huko ulipo ukipwaya kidogo itakuwa kama ya Yondani jina lake halitosahaulika Katika soka la Tanzania ambae alieinyanyua Yanga kuifikisha kileleni kwa miaka kadhaa, yukowapi leo
ReplyDeleteHuyu tunampeleka Namungo sio Yanga kwenye njaa...Tunampeleka kwa PM tunajua atakuwa anapandisha kiwango na kuja kuisaidia Simba baadae.
ReplyDeleteMbona hamshauri Raphael Daudi wa Yanga ahame ili kulinda kipaji chake. Raphael ambaye alicheza mpaka timu ya Taifa?Au huruma ya machozi ya mamba?
ReplyDeleteHakuna mtu aliyemshauri ahame Simba aje Yanga. Tumesoma Haruna Niyonzima alitoa ushaur kwa Ndemla alipohojiwa na mwandishi wa habari kuhusu performance ya Ndemla na anavyoendelea kukaa benchi. Suala la kuhama ni lake na hakuna mtu wa kumlazimisha. Kwani mtu akitoa maoni yake ni lazima yafuatwe na mhusika?
DeleteAngeanza kuwashauri walio timu moja na yeye(mshauri)Ndemla hamhusu kitu.
ReplyDelete