UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mashabiki wajitokeze kwa wingi kuwapa sapoti watakaposhuka Uwanja wa Majaliwa kusaka pointi tatu mbele ya Namungo FC.
Yanga iliyo chini ya Kocha Mkuu, Luc Eymael itamenyana na Namungo leo Uwanja wa Majaliwa ikiwa na kumbukumbu ya kuchapwa bao 1-0 na KMC kwenye mchezo wao wa ligi uliopita.
Ofisa Habari wa Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa wanatambua utakuwa mchezo mgumu lakini wamejipanga kupata matokeo chanya.
"Tunatambua utakuwa mchezo mguu ila tupo tayari kuona tunapata ushindi, mashabiki wajitokeze kwa wingi leo kutupa sapoti tunazihitaji pointi tatu," amesema.
Huu unakuwa ni mchezo wa kwanza kuwakutanisha wapinzani hawa ndani ya Ligi Kuu Bara baada ya Namungo FC kupanda daraja msimu huu wa 2019/20.
Piga hao vyura ndumba fc hawana lolote katika soka ni mabwege tu!
ReplyDeleteIngekuwa ni Simba wachezaji wamegoma kwenda Ruangwa kwenye mechi na Namungo zingeandikwa makala zaidi ya 5.Ila timu pendwa kimyaa. Luc analalamika kwambwa wachezaji hawaonyeshi weledi.
ReplyDelete