UONGOZI wa Azam FC umesema kuwa ni wakati wa nahodha wa Simba, John Bocco kurejea Azam FC kwa kuwa ndio maskani yake ilipo.
Bocco alijiunga na Simba msimu wa 2017 akitokea Azam FC yenye maskani yake Chamazi.
Ofisa Habari wa Azam FC, Zaka Zakazi amesema kuwa ni wakati sahihi wa nyota huyo kurejea Azam kuendelea na soka.
"Bocco ni mchezaji mzuri na ana uwezo mkubwa akiwa uwanjani kwani anachokifanya kinaonekana, kwa sasa ni wakati wake kurejea Azam FC ili kurejea nyumbani," amesema.
Msimu huu ndani ya Simba, Bocco amefunga mabao manne na kutoa pasi mbili za mabao.
Mlimtemea nini na sasa mnamtakia nini. Boco ni uti wa mgongo wa Simba. Hakuna atachoweza kwengine akakikosa kwa Moo. Vipi utaitaja Simba Bila ya kumtaja Bocco na vipi utamtaja Bocco Bila ya kutaja Simba. Hands in gloves
ReplyDeleteAzam hamjawahi kujielewa, mnaelea vipaji halafu mnavitupa mnaishia kuikomoa yanga. Hivi kweli unaweza kumuacha boko ukaenda kumchukua Ngoma majeruhi? Azam kama mgekuwa na mipango sahihi msingekuwa wa kuvizia wachezaji wa Simba na Yanga, leo hii mlitakiwa muwe kwenye level za akina mazembe, Al Ahal nk.
ReplyDelete