April 11, 2020

WADHAMINI wa Yanga, Kampuni ya GSM wamerejea kivingine klabuni hapo na safari hii wamekuja na staili mpya ya usajili kwa wachezaji wa kimataifa ambayo ili usajiliwe ni lazima uichezee timu ya taifa ya nchi yako.

Hiyo ikiwa ni siku chache tangu GSM watangaze kurejea kuendelee na udhamini wa nje ya mkataba ikiwemo posho, mishahara wa wachezaji na benchi la ufundi, kambi za wachezaji na usajili ambayo ilifanikisha usajili wa Bernard Morrison, Haruna Niyonzima, Ditram Nchimbi, Yikpe Gnaimen.

GSM imerejea Yanga ni baada ya hivi karibuni kutangaza kujiondoa kwenye udhamini wa timu hiyo kufuatia baadhi ya viongozi wa Kamati ya Utendaji kudai wadhamini hao wanaingilia majukumu ya viongozi likiwemo suala la usajili.

Mwenyekiti wa Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa kwa sasa wataendelea kufanya ushirikiano na GSM kwa kuwa ni wanafamilia na wanaipenda timu ya Yanga.

"GSM ni wanafamilia wa Yanga wanaipenda timu ndio maana wapo nasi bega kwa bega, wamekuwa nasi kwenye nyakati mbalimbali na wamefanya makubwa ikiwa ni pamoja na kutupa sapoti wakati wa kambi pale Tanga tulipocheza na Coastal Union hivyo bado kuna tupo nao pamoja," amesema.

7 COMMENTS:

  1. Wanachokifanya GSM kimebarikiwa na wananchi wenye timu yao au ni utashi wa viongozi peke yao ili wafukuzane wanaohoji ushirikishwaji wa wenye timu yao?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nyie kwa Mo na bill 20 uchwara mmeshirikishwa, mnajua hata ziliko? acheni wivu. Mtu anayekupa msaada haitaji kukushirikisha, ni ukitaka pokea au ukitaka acha

      Delete
    2. Punguza povu brother,na pia kumbuka MO DEWJ sio mdhamini wa club simba maana tafsiri ya mdhamini hapati chochote kitu katika udhamin wake,mfano hata wewe unaweza ukamdhamin mtu akachukua mkopo kwenye taasisi za fedha lakin mwisho wa siku hazitakusaidia wewe mdhamin bali yeye anaekopa,MO DEWJ ni muwekezaji tena kwa mfumo wa hisa kaa ukijua uwekezaji hasa katika michezo ni suala la mchakato kamwe usitarajie majibu ya haraka,maana yangu ni kwamba wengi mnataka muione simba ya tofauti bila yakuzingatia muda ambao muwekezaji amepewa nafasi,hapa watakaonielewa ni watu wenye utashi mkubwa kidogo katika masuala ya uwekezaji wa muda mrefu,simba itakuja kua taasisi kubwa sana miaka ijayo endapo tu watafanya kama wanavyonadi nakuhubiri,na bila yakupepesa macho haya yanayofanyika yanga kupitia kwa mdhamin G.S.M hayakuanza leo wale waliokuwepo miaka ya nyuma wataniunga mkono,kwa maana yatakwisha au yatakua na kikomo,kudhamin timu bila ya kua na ingizo ni ngumu sana yani yanga iwe inatumia tu pesa za GSM alafu mapato wanachukua klabu wenyewe,hapo tunadanganyana bhana lazima itumike role WE CONSUME WHAT WE PRODUCE na ikiwa kinyume ujue italeta madhara tu baada wana historia watanipa 5 hapa,yanga lazima tukubali kutafuta namna yakubadili mfumo ili tuweze kupiga hatua za kimaendeleo katika soka.please povu haturuhusu.

      Delete
    3. Ulichokiandika hata hukitambui. Yanga ipo na GSM na inaweka mikakati ya kujitegemea na kuwa timu yenye mfumo mzuri wa kiuendeshaji kama vilivyo vilabu vikibwa ulimwenguni. Simba MO aliahid kuwapa Bilioni 20 na hajatoa ni porojo tu. Sisi GSM anafanya mambo ya kuisaidia klabu kama mwqnachama, lakini MO ni mwekezaji na mlimpa uwekezaji kwa ahadi yankuwapa bilioni 20. Hamuoni kuwa mnadanganywa?

      Delete
  2. The time will tell brother usije ukaja kutafutwa kwa tochi bila mafanikio,GSM hana muda hapo na kama unabisha subiri uone yajayo muda sio mrefu.

    ReplyDelete
  3. Investiment haiko hivyo unavyodhani,wewe ulitaka mo alete pesa mezani awape akina nani sasa?ikiwa yeye ndio mwenye timu na ndio anaefanya coverege ya costs zote zinazohusu timu,bilioni 20 sio takrima ni pesa inayoingia kwenye investiment na sio wapewe watu wapige wasepe zao jaribu kuelewa basi hata kwakukariri.

    ReplyDelete
  4. Ingekuwa billion 20 sio za kuweka kwenye account maalum, Basi hata mwenyekiti alieondoka asinge hoji, Kama utakumbuka MO alivyosema anajitoa,anasema amesha tumia 4 billions, Kigwangala aliuluza hizo 4B zipo ktk zile 20.
    Kiufupi hizo 20 billions bado hazina ufafanuzi na mwisho wasiku Kuna possibilities ya watu kulizwa...

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic